KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI

KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI
kiungo : KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI

soma pia


KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Charles Kabeho akiongea na mkuu wa wilaya ya Rufiji Juma Njwayo ,wakati akikagua wodi ya watoto ikiwa ni sehemu ya majengo ya mradi wa kituo cha afya cha Ikwiriri ,Rufiji, mkoa wa Pwani.

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

KIONGOZI wa mbio za mwenge mwaka huu, Charles Kabeho ,amekataa kuzindua mradi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani.

Hali hiyo imezua sintofahamu mara baada ya kusomwa ripoti ya matumizi ya fedha ambazo hazijaeleweka zimetumikaje huku serikali ikiwa imechangia kiasi cha sh.milioni 400.

Aidha  kwa mujibu wa taarifa ya wilaya imedaiwa wananchi wamechangia milioni tatu wakati taarifa ya mkoa inaonyesha ilichangia milioni moja.

Akizungumza kwenye kituo hicho cha afya, Kabeho alishtushwa na kuhoji kutokea kwa hali hiyo.

Alimtaka mkuu wa wilaya atoe kauli yake na kukataa kuuzindua mradi mpaka watakapotoa taarifa ya uhakika.

Kabeho aliasa halmashauri na wilaya mbalimbali ,kusimamia miradi ya maendeleo ili iendane na thamani halisi ya fedha .

Nae mkuu wa wilaya  ya Rufiji,Juma Njwayo aliviagiza vyombo vya ulinzi na usalama hususani taasisi ya kupambana na rushwa (TAKUKURU) kufuatilia suala hilo.

Kati ya miradi tisa ambayo ilipaswa kukaguliwa,kuwekwa jiwe la msingi na kuzinduliwa wilayani Rufiji ,iliyogharimu bilioni 2.654.40 mradi huo mmoja ulikwama kuzinduliwa .

July 13 mwenge huo ulikuwa Rufiji na July 14 umetembelea miradi ya maendeleo katika wilaya ya Kibiti.


Hivyo makala KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI

yaani makala yote KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/kabeho-akataa-kuzindua-mradi-wa-kituo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KABEHO AKATAA KUZINDUA MRADI WA KITUO CHA AFYA IKWIRIRI"

Post a Comment