title : Jeshi la Polisi Kilimanjaro Lafanya Ukaguzi wa Leseni za Madereva 2000.
kiungo : Jeshi la Polisi Kilimanjaro Lafanya Ukaguzi wa Leseni za Madereva 2000.
Jeshi la Polisi Kilimanjaro Lafanya Ukaguzi wa Leseni za Madereva 2000.




Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limekagua Leseni za Madereva 2182 ,madereva 13 wakibainika kutumia Leseni za madaraja yasiyoruhusu kuendesha Magari ya Abiria huku Madereva watatu wakishikiliwa kwa kosa la kuendesha gari bila ya kuwa leseni.
Katika ukaguzi huo uliofanyika kwa muda wa wiki moja katika mkoa wa Kilimanjaro ,Jeshi la Polisi pi limebaini uwepo wa madereva waliovuka umri wa kuendesha gari kwa mujibu wa sheria ambao ni miaka 60 huku likiwataka kuacha mara moja kuendelea na kazi hiyo.
Kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyobainika kwa Madereva wa Magari ya Abiria ,Jeshi la Polisimkoa wa Kilimanjaro likatangaza kuanza mafunzo kwa Madereva wa magari ya Abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni pamoja na maelekezo ya alama mpya za barabarani.
Akizungumza kwa niaba ya Madereva,Dereva mzoefu wa magari makubwa ,Apolonary Malya amepongeza utaratibu huo wa jeshi la Polisi kutoa mafunzo ikiwa ni sehemu ya kuwakumbusha madereva baadhi ya sheria ya usalama barabarani.
Mafunzo kwa madereva hao yameanza kutolewa katika ukumbi mdogo uliopo ofisi za kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa kikosi hicho Mrakibu msaidizi wa Polisi Zauda Mohamed na maofisa wengine wa Polisi .
Mwisho .
Hivyo makala Jeshi la Polisi Kilimanjaro Lafanya Ukaguzi wa Leseni za Madereva 2000.
yaani makala yote Jeshi la Polisi Kilimanjaro Lafanya Ukaguzi wa Leseni za Madereva 2000. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jeshi la Polisi Kilimanjaro Lafanya Ukaguzi wa Leseni za Madereva 2000. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/jeshi-la-polisi-kilimanjaro-lafanya.html
0 Response to "Jeshi la Polisi Kilimanjaro Lafanya Ukaguzi wa Leseni za Madereva 2000."
Post a Comment