IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI

IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI
kiungo : IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI

soma pia


IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewasili mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi na Julai 5 mwaka huu anatarajiwa kufunga mafunzo katika Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza ambayo yana lengo la kukabiliana na uhalifu unaotokea katika Bahari, Maziwa na Mito hapa nchini.
Pamoja na ufungaji wa mafunzo hayo pia ataendelea na ziara ya kukagua utendaji wa Polisi katika baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa lengo la kuhakikisha uhalifu unapungua  hapa nchini ikiwemo ajali za barabarani, Maujai ya kishirikina na uhalifu katika Visiwa vilivyopo Ziwa Viktoria.
Mapema baada ya kuwasili amezungumza na Maofisa wa Polisi waliopo Mkoani Mwanza na kusisitiza kufanya kazi kwa weledi pamoja na kuhakikisha kuwa ajali zinapungua katika maeneo yao.
“Nimekuja kukagua utendaji wenu ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili ili kufikia malengo tuliyojiwekea ya kuhakikisha uhalifu unapungua hapa nchini, hivyo ni imani yangu kila mmoja atawajibika kwa nafasi yake na kuwasimamia waliopo chini yake ipasavyo” Alisema IGP Sirro
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ahmed Msangi amesema hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari na suala la usalama barabarani linaendelea kusimamiwa kikamilifu kwa kushirikiana Mamlaka nyingine zinazohusika.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi  kwenye baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmed Msangi (Kulia) na Afisa Mnadhimu wa Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera Bulimba (Kulia) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya kikazi kwenye baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea Salam ya heshima baada ya kuwasili Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Mwanza kwa ziara ya kikazi katika baadhi ya mikao ya Kanda ya Ziwa.Kushoto ni Kamanda wa mkoa huo, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ahmed Msangi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimfariji Bi Lily Matola ambaye ni Afisa Mnadhimu Mstaafu wa Polisi mkoani Mwanza baada ya kufiwa na Mume wake Marehemu Edmund Matola. IGP Sirro yupo ziara ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuangalia utendaji wa Polisi hususani katika kupunguza ajali za barabarani nchini.
Habari na Picha na Jeshi la Polisi


Hivyo makala IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI

yaani makala yote IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/igp-sirro-awasili-mwanza-kwa-ziara-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "IGP SIRRO AWASILI MWANZA KWA ZIARA YA KIKAZI KANDA YA ZIWA, KUFUNGA MAFUNZO CHUO CHA POLISI WANAMAJI"

Post a Comment