Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja

Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja
kiungo : Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja

soma pia


Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM


KIUNGO Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye mchana wa jana ametambulishwa na Singida United – jioni hii ametangazwa Yanga kwamba amejiunga na kwa mkataba wa miaka mitatu.



Fei alikuwepo makao makuu ya klabu ya Yanga akiwa na jezi ya klabu huyo na kutambulishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika kama mchezaji mpya wa klabu hiyo pamoja na kiungo mwingine, Jaffar Mohammed kutoka Maji Maji ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.

Feisal hakutaka kuzungumza chochote kuhusu kuonekana anatambulishwa na Singida United, lakini Meneja wa JKU, Mohammed Kombo aliyekuwapo mkutanoni pia amesema kwamba Yanga imekamilisha taratibu za kumchukua mchezaji huyo.



Mapema leo, Singida United imemtambulisha Fei Toto kwa kutoa picha akisaini mkataba na kukabidhiwa jezi ya timu hiyo. 

Na katika taarifa yake, Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Zanzibar amesaini mkataba wa miaka mitatu.

Sanga alisema kwamba Fei alikuwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa JKU, lakini walizungumza na klabu yake na kufikia makubaliano ya kuununua mkataba huo. 

Bado haijulikani nini kimejificha nyuma ya usajili wa Fei Toto – baada ya kuonekana anasaini Singida United asubuhi na jioni hii anaibukia Yanga.


Lakini kwa mujibu wa kanuni za usajili, iwapo itagundulika Fei amesaini mikataba na timu zote, atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufungiwa kuanzia mwaka mmoja.


Hivyo makala Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja

yaani makala yote Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/fei-toto-asajili-siongida-united-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Fei Toto asajili Siongida United na Yanga kwa siku moja"

Post a Comment