title : SERIKALI YAKARABATI SHULE ZAKE KONGWE ZA SERIKALI ILI KUBORESHA ELIMU
kiungo : SERIKALI YAKARABATI SHULE ZAKE KONGWE ZA SERIKALI ILI KUBORESHA ELIMU
SERIKALI YAKARABATI SHULE ZAKE KONGWE ZA SERIKALI ILI KUBORESHA ELIMU
Na Benny Mwaipaja, WFM, Kibaha
Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni 42 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya Sekondari 42 kati ya shule 88 kongwe zilizopo nchini kote ikiwemo shule ya Sekondari Ruvu iliyoko Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza mara baada ya kukagua ukarabati wa shule hiyo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa shule zote Kongwe ambazo zinahistoria kubwa ya kutoa viongozi wengi na wataalam mbalimbali nchini, zinakuwa na hadhi na kuwa kimbilio la wananchi.
Ametoa wito kwa uongozi wa shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ili thamani ya uwekezaji mkubwa wa Serikali unaofikia zaidi ya shilingi milioni 990 uweze kuonekana
"Dhamira yetu ni kuona watoto wetu wanasoma kwenye mazingira sahihi na ufaulu wao unaongeeaka kwa sababu tunawaandaa wataalam wa kesho wa Taifa letu" Aliosisitiza Dkt. Kijaji
Alisema amejionea ukarabati uliofanyika shuleni hapo ambapo pamoja na shilingi milioni 992 kutumika katika ukarabati huo, bado nyumba 6 za walimu hazijakarabatiwa pamoja na kutonunuliwa kwa samani za shule vikiwemo vitanda na kuahidi kuifanyia kazi changamoto hiyo wakati wa huu wa mchakato wa bajeti mpya
Kwa upande wao, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Hamoud Juma na Mkuu wa Shule hiyo, Juliana Chimazi, wameishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha shule hiyo na kuomba wapatiwe fedha kwa ajili ya kununulia samani hasa vitanda kwa ajili ya wanafunzi ili kwenda sambamba na uboreshaji mkubwa wa majengo uliofanyika shuleni hapo.
Mkuu wa shule hiyo Mwl. Juliana Chimazi alimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji kwamba shule hiyo inahitaji vitanda vipya kwa kuwa vilivyopo vimedumu zaidi ya miaka 50 pamoja na kuomba fedha kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa nyumba sita za walimu.
Miongoni mwa miundombinu iliyoboreshwa katika shule hiyo ya Sekondari ya washichana Ruvu ni pamoja na mifumo ya maji taka, madarasa, vyoo, mabweni, nyumba za walimu na Ofisi.
Naibu Waziri Dkt. Kijaji anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali iliyopewa fedha na Serikali ikiwemo ya kimkakati inayolenga kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kujitekemea kwa mapato.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa viongozi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu Mkoani Pwani, kuhakikisha maboresho ya shule hiyo yanakwenda sambamba na ufanisi katika utoaji taaluma, wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua uboreshaji huo. Kulia ni Mbunge wa Kibaha Vijijini Mhe. Hamoud Juma na kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akikagua maboresho ya Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, wa pili kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kibaha Bi. Fatuma Kisanazo, watatu kushoto ni Mbunge wa Kibaha Vijijini Mhe. Hamoud Juma na kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi.
Muonekano wa Bweni la wanafunzi wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, ambapo Mkuu wa Shule hiyo Bi. Juliana Chimazi, aliomba Serikali isaidie katika kuboresha miundombinu ya nyumba 6 za walimu ambayo haijakarabariwa baada ya fedha sh. milioni 990 kumalizika kabla ya kazi hiyo kukamilika.
Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Kibaha Bi. Fatuma Kisanazo, akitoa ufafanuzi wa namna walivyosimamia fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya kuboresha Shule Kongwe ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, wakati wa ziara yua kikazi ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani Bw. Shaibu Mangalu, akielezea namna Shule hiyo ilivyotumia utaratibu wa shule hiyo kwa njia ya Force Account uliogharimu takribani Sh. milioni 992, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipotembelea na kukagua maboresho hayo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Viongozi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Ruvu, Mkoani Pwani, ,baada ya kukagua uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo .Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango).

Hivyo makala SERIKALI YAKARABATI SHULE ZAKE KONGWE ZA SERIKALI ILI KUBORESHA ELIMU
yaani makala yote SERIKALI YAKARABATI SHULE ZAKE KONGWE ZA SERIKALI ILI KUBORESHA ELIMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAKARABATI SHULE ZAKE KONGWE ZA SERIKALI ILI KUBORESHA ELIMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/serikali-yakarabati-shule-zake-kongwe.html
0 Response to "SERIKALI YAKARABATI SHULE ZAKE KONGWE ZA SERIKALI ILI KUBORESHA ELIMU"
Post a Comment