title : DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI
kiungo : DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI
DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI
Tarime - Mara
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Jeshi la Polisi wilaya ya Tarime mkoani Mara kumkamata na kumfungulia mashtaka Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya hiyo, Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Richard Tiboche kwa tuhuma za kuikashifu Serikali na kuchochea mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi ya Serengeti na vijiji jirani.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana majira ya saa tatu usiku baada ya kuhitimisha ziara yake wilayani humo iliyolenga kutafuta suluhu ya mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani ikiwemo kijiji cha Kegonga.
Akiwa njiani majira ya saa tatu za usiku kwenye gari la wazi baada ya kukagua eneo hilo la mpaka kwa zaidi ya masaa sita, Waziri Kigwangalla na msafara wake walikuta lundo la mawe yakiwa barabarani ndani ya eneo la hifadhi hiyo, hali iliyosababisha taharuki kubwa na msafara wake kushuka na kuanza kuondoa mawe hayo ili kupata njia ya kupita.
Wakati zoezi hilo likiwa linaendelea, Kiongozi huyo wa UVCCM alisikika akiituhumu Serikali kwa kuweka mawe hayo na kwamba hayakuwekwa na wananchi wa eneo hilo, jambo lililozua mshangao mkubwa kwa viongozi wa Serikali waliokuwepo katika msafara huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima mtego wa misumari uliotegwa na watu wasiojulikana kwa lengo la kuzuia msafara wake wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Tarime John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa eneo lenye mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro huo mkoani Mara jana. Katikati aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa huo, Adam Malima.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma taarifa mbalimbali kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani vya wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kutatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji na hifadhi hiyo jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche.
Hivyo makala DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI
yaani makala yote DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/dk-kigwangalla-aagiza-katibu-wa-uvccm.html
0 Response to "DK. KIGWANGALLA AAGIZA KATIBU WA UVCCM TARIME KUKAMATWA NA KUFUNGULIWA MASHTAKA YA KUIKASHIFU SERIKALI"
Post a Comment