title : CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAANZA KUDAHILI WANAFUNZI 2018/2019
kiungo : CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAANZA KUDAHILI WANAFUNZI 2018/2019
CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAANZA KUDAHILI WANAFUNZI 2018/2019
Na Leandra Gabriel, Blogu jamii
CHUO cha Ustawi wa Jamii kilichopo Kijitonyama jijini Dar es salaam kimeanza kudahili wanafunzi kwa mwaka 2018/2019 katika maonesho al maarufu kama maonesho ya TCU yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Akizungumza na Michuzi blog Msajili wa Chuo hicho Nuru Kalufya ameeleza kuwa katika kupokea wanafunzi katika msimu huu na wanasajili kupitia mtandao (online) bure na kinachohitajika ni wanafunzi kuwa na vyeti vyao na namba zao za usajili (index number) na watapata huduma hiyo ya udahili na ushauri wa kitaaluma bure kabisa.
Kuhusu kozi zinazotolewa na Chuo hicho bi. Nuru ameeleza kuwa wanatoa kozi tano kwa gharama nafuu kabisa na hii ni kuanzaia ngazi ya cheti, stashahada, shahada, uzamili na post graduate ya kozi ya Health System Management ambayo ni mpya kabisa chuoni hapo.
Akizungumzia kuhusiana na usajili wa Chuo Nuru amesema kuwa wamesajili na wanatambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) pamoja na NACTE na Serikali kwa ujumla.Hivyo wazazi na wadahiliwa wasiwe na hofu.
Aidha ameeleza kuwa watatoa huduma katika maonesho hayo hadi kesho majira na saa kumi na moja jioni na baadaye wataendelea kutoa huduma hizo katika chuo chao kinachopatika Kijitonyama hivyo wanafunzi waendelee kujitokeza kwa wingi zaidi.
Kwa upande wake Mshauri wa wanafunzi bi. Silvia Ngiga amewahakikishia wanafunzi usalama pindi wawapo shuleni na wanafunzi watokao mikoani watapata za malazi na huduma nyingine za kijamii ni za kuaminika katika chuo hicho.
Msajili wa Chuo cha ustawi wa jamii Nuru Kalufya akizungumza na blogu ya jamii kuhusu mikakati walioweka katika kudahili wanafunzi wapya 2018/2019
Mshauri wa wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa jamii Silvia Ngiga akizungumza na Michuzi blog kuhusiana na maonesho katika maonesho ya TCU yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Hivyo makala CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAANZA KUDAHILI WANAFUNZI 2018/2019
yaani makala yote CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAANZA KUDAHILI WANAFUNZI 2018/2019 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAANZA KUDAHILI WANAFUNZI 2018/2019 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/chuo-cha-ustawi-wa-jamii-chaanza.html
0 Response to "CHUO CHA USTAWI WA JAMII CHAANZA KUDAHILI WANAFUNZI 2018/2019"
Post a Comment