POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO

POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO
kiungo : POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO

soma pia


POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limeendesha mafunzo kuhusu masuala ya usalama barabarani kwa wamiliki na madereva wa magari,pikipiki na bajaji ikiwa ni sehemu ya njia za kukabiliana na ajali zinazojitokeza na kusababisha vifo na majeruhi. 

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro yamefanyika leo Alhamis Julai 12,2018 katika ukumbi wa Bwalo la Polisi mjini Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema suala la utii wa sheria za barabarani ni jukumu la watu wote hivyo kila mmoja lazima azingatie sheria za barabarani ili kuepuka ajali zisizo za lazima.

"Madereva ni wadau wakuu wa kuzuia ajali za barabarani, nalipongeza jeshi la polisi kwa kuona umuhimu na wadau hawa ili kuwapa elimu hii kwani madereva wakisikiliza na kufanyia kazi elimu hii hakika ajali hazitatokea mkoani Shinyanga",alieleza Matiro.

"Ili kutokomeza ajali,ni vyema jeshi la polisi likaendelea kufanya doria katika barabara kuu, kukagua leseni na kuhakikisha magari yote mabovu hayaiingii barabarani lakini pia kutoa elimu kwa wadau wote wakiwemo wanafunzi",aliongeza Matiro.
Kulia ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akimuonesha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ratiba ya mada zinazofundishwa kwa wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya moto ikiwemo magari,pikipiki na bajaji.
Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Shinyanga SSP Richard George Abwaoakiteta jambo na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga ASP Anthony Gwandu.
Dereva na mmiliki wa Tax na pikipiki, Omari Gindu akiomba askari wa usalama barabarani 'Trafiki' nao wapewe elimu ya usalama barabarani akidai baadhi yao hawajui sheria hivyo kukamata ovyo madereva na kuchangia kutokea kwa ajali
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akisisitiza kuwa jeshi la polisi litaendelea kuwachukulia hatua za kisheria madereva watakaokiuka sheria za usalama barabarani.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro . Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Shinyanga SSP Richard George Abwao
Madereva na wamiliki wa vyombo vya moto wakiapa kuzingatia sheria za barabarani ili kutokomeza ajali mkoani Shinyanga.



Hivyo makala POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO

yaani makala yote POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/polisi-shinyanga-yatoa-elimu-ya-usalama.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "POLISI SHINYANGA YATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO"

Post a Comment