WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA

WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA
kiungo : WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA

soma pia


WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA




WAZIRIMKUU Kassim Majaliwa amewataka wataalamu wa sekta za kilimo, mifugo na maji watumie taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili waongeze ufanisi katika utendaji kazi wao.


Amesemakuwa kuongezeka kwa vituo vipya vya kisasa vya ufuatiliaji wa mwenendo wa hali ya hewa kumeboresha uhakika wa utabiri kutoka asilimia 81 hadi 87 kama inavyoshuhudiwa kwenye taarifa zinazotolewa katika siku za hivi karibuni. “Hivi sasa tukiambiwa kwamba mvua itanyesha katika maeneo fulani tunakuwa na uhakika kwa asilimia 87 ya utabiri huo,”. 

Vituo hivi ni muhimu katika kuimarisha uwezo wa nchi wa utoaji wa huduma za hali ya hewa na haidrolojia kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuongeza ufanisi katika utoaji wa tahadhari za awali za majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi,”. 

Amesema kupitia mradi huo uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Serikali imeweza kufungua vituo 51 vya kisasa vya hali ya hewa katika maeneo mbalimbali nchini na vituo 15 vya kupima ujazo wa maji kwenye mito iliyopo kwenye mabonde ya Pangani, Ruvuma na Pwani ya Kusini ambavyo vinajiendesha vyenyewe. 

“Pia, mradi huu umeiwezesha Serikali kuanzisha kanzidata ya takwimu na taarifa za mafuriko         na ukame na taarifa za hali ya hewa na kuondoa ucheleweshwaji wa kupata takwimu au taarifa kutoka Wizara moja kwenda Wizara nyingine,” amesema. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano zitenge fedha kwenye bajeti zao ili ziweze kufuatilia na kusimamia mradi huo baada ya wafadhili kumaliza muda wao.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa vituo na mifumo iliyowekwa inafanya kazi ipasavyo kwa usimamizi bora ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.

Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola, Wabunge na Mwakilishi Mkaazi wa Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bibi Natalie Boucly.



Hivyo makala WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA

yaani makala yote WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wataalamu-tumieni-taarifa-za-tma.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATAALAMU TUMIENI TAARIFA ZA TMA-MAJALIWA"

Post a Comment