title : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BARAZA LA EID KITAIFA MKOANI KILIMANJARO
kiungo : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BARAZA LA EID KITAIFA MKOANI KILIMANJARO
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BARAZA LA EID KITAIFA MKOANI KILIMANJARO
*Ahimiza nyumba za ibada zisaidie vita ya dawa za kulevya
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi kuanzia leo. “Kuanzia leo, ni marufuku kwa mtu yoyote kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi bila ya vibali. Serikali inahamasisha uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda nchini. Kama tutatoa vibali, ni lazima mtu alazimike kusaga nafaka ili kutoa ajira nchini,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 26, 2017) wakati akitoa nasaha kwenye Baraza la Eid lililofanyika kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuswali sala ya Eid.
“Jana nimeona kwenye televisheni taarifa kuhusu malori 10 yaliyokamatwa Tarakea yakiwa na mahindi tayari kuvushwa mpaka. Mheshimiwa RC akasema chakula hicho ni lazima yarudishwe kwa ajili ya usagaji.”
“Mimi nasema kuanzia leo, yeyote atakayekamatwa akitorosha chakula kwenda nje ya nchi, chakula hicho kitataifishwa na kupelekwa ghala la Taifa na gari lake tutalitaifisha na litaishia Jeshi la Polisi. Tunafanya hayo kwa lengo la kuwalinda Watanzania tusikumbwe na baa la njaa.”
Akitoa tahadhari kuhusu uuzwaji wa chakula nje ya nchi, Waziri Mkuu amesema kumekuwa na wimbi kubwa la usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi bila kibali. “Hilo ni kosa kubwa kwa sababu litasababisha nchi yetu kupata baa la njaa huko mbele,” amesema.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa nasaha kwa waumini (hawapo pichani) waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa nasaha za Eid, tarehe 26 Juni, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally wakati wa stafutahi kwenye Ikulu ndogo ya Moshi, mara baada ya Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally mara baada ya stafutahi kwenye Ikulu ndogo ya Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Hivyo makala WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BARAZA LA EID KITAIFA MKOANI KILIMANJARO
yaani makala yote WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BARAZA LA EID KITAIFA MKOANI KILIMANJARO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BARAZA LA EID KITAIFA MKOANI KILIMANJARO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-ahutubia.html
0 Response to "WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA BARAZA LA EID KITAIFA MKOANI KILIMANJARO"
Post a Comment