title : Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili
kiungo : Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili
Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akikabidhi zawadi ya kikombe kwa Idara ya upasuaji ambayo imekuwa mshindi wa kwanza kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yalianza tarehe 18 hadi 20 Juni, 2018 kwenye viwanja vya Muhimbili. Idara hiyo imepatiwa zawadi ya kikombe, fedha na cheti cha ushiriki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akishuhudia shughuli ya kukabidhi zawadi kwa washiriki mbalimbali. Mwenyekiti huyo amefunga maonesho ya siku tatu yalioanza tarehe 18 hadi 20, Juni 2018 kwenye viwanja vya Muhimbili. Wengi walijitokeza kupima afya BURE, kupata elimu na ushauri kuhusu afya zao.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dkt. Juma Mfinanga akipokea zawadi ya kikombe kutoka kwa Prof. Majinge. Pia, Idara hiyo imepatiwa fedha na cheti cha ushiriki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru.
Wananchi wakitembelea banda la Magonjwa ya Damu na Saratani za Damu katika maonesho yaliofanyika Muhimbili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akikabidhi zawadi ya fedha na kikombe kwa Idara meno.
Idara ya macho nayo haikuwa nyuma katika kutoa huduma bora kwa wananchi waliofika kwenye banda lao kwani walishinda kikombe pamoja na feda taslimu.
Hivyo makala Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili
yaani makala yote Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/washiriki-washinda-vikombe-fedha.html
0 Response to "Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili"
Post a Comment