SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI

SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI
kiungo : SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI

soma pia


SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI

SERIKALI imewataka wananchi kuunga mkono juhudi za usafi kwa kunawa mikono na sabuni ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu ili kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora.

Akizungumza katika kilele cha wiki ya unawaji mikono kwa maji na sabuni iliyofanyika Kata ya Kiwalani, Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Ubora wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASA), Dk Sufiani Masasi alisema kama Taifa ni muhimu kuwekeza nguvu katika kuelimisha jamii hasa umuhimu wa kunawa mikono na majisafi na sabuni ili kujenga Taifa lenye afya bora.

Akizungumza na jumuiya ya wananchi, waalimu na wanafunzi wa shule za msingi Umoja, Yombo, Mwale na Bwawani, Dk Masasi alisema DAWASA ni mdau muhimu wa usafi wa mazingira ndio sababu waliamua kuadhimisha wiki hiyo kwa kutoa elimu kwa walimu 44 kutoka katika shule hizo pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa ili wawe mabalozi
wazuri katika kuwaelimisha wanafunzi juu ya umuhimu wake.

Alisema kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni ‘Mikono safi kwa manufaa ya sasa na baadae’ inaikumbusha jamii kuona umuhimu wa kunawa mikono na sabuni ili kujikinga na maradhi yatokanayo na uchafu.

Hivyo alitaka juhudi za pamoja zichukuliwe kuhakikisha wanafunzi wanaelewa umuhimu wa kunawa mikono kwani wao ndio wazazi wa siku zijazo na kwamba DAWASA itaendelea kuunga mkono kampeni za usafi hasa kwa kuendelea kubuni na kutengeneza miundombinu ya majisafi katika Maeneo mbalimbali ya jiji.

Dk Masasi alisema tayari DAWASA imefanikiwa kufikisha mradi huo wa majisafi kwa shule hizo ambapo utanufaisha wanafunzi 5123 pamoja na zahanati ya eneo hilo na kwamba itaendelea kufadhili miradi ya aina hii ili kuunga mkono juhudi hizo za usafi wa mazingira.

Mkufunzi wa mafunzo kwa walimu wa shule hizo, Juhudi Nyambuka ambaye ni Afisa Afya Manispaa ya Temeke alipongeza juhudi za DAWASA katika kusaidia jamii kupata huduma za majisafi na kueleza zitasaidia kupunguza magonjwa yanayosababishwa na ukosefu wa maji.

Katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma rasmi za maji ya bomba DAWASA, jumuiya za wananchi pamoja na wadau wa maendeleo wamekuwa wakijenga miradi ya maji kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira kwa jamii. 

Miradi hiyo ipo katika maeneo mbalimbali kama vile Ukonga, Yombo, Kitunda, Mbagala, Kijichi, Feri,Kigamboni.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Wanafunzi wa Shule za Msingi zilizopo Kata ya Kiwalani wakishiriki igizo lenye lengo la kuelimisha jamii umuhimu wa kunawa mikono na majisafi na sabuni wakati wa kilele cha wiki ya unawaji mikono kwa maji na sabuni yaliyofanyika Kiwalani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Hivyo makala SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI

yaani makala yote SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/serikali-yahimiza-unawaji-mikono-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAHIMIZA UNAWAJI MIKONO NA SABUNI"

Post a Comment