title : WAMTAKA WAZIRI WA MADINI AIRUKI KUINGILIA KATI SUALA LAO
kiungo : WAMTAKA WAZIRI WA MADINI AIRUKI KUINGILIA KATI SUALA LAO
WAMTAKA WAZIRI WA MADINI AIRUKI KUINGILIA KATI SUALA LAO
Wakati Serikali ya awamu ya Tano Ikijinasibu kwa mapambano ya Rushwa bado imeonekana kwa watendaji kwenye sekta ya Madini kanda ya kati kukiuka sheria ya madini ya mwaka 2010 rejeo lake mwaka 2017 kwa kuwakandamiza wachimbaji wadogo na kuipa Kampuni ya Kondoa Minningi eneo la wachimbaji kinyume na sheria hizo ambapo kampuni hiyo imekuwa na ubia na kampuni kutoka Nchi jirani Kinyume na sheria.
Sakata hilo lililodumu kwa mwaka sasa huku ofisi za madini kanda na ofisa madini mkazi Dodoma kutupiana mpira bila majibu ambapo wachimbaji hao waliomba maombi halali kama serikali inavyotaka tokea mwaka 2015 mwezi 3 tarehe 12 bado mpaka mda huu majibu kwa wachimbaji hao yamekuwa kizungumkuti huku mamlaka mbali mbali zikiwa kimya bila majibu ambapo wamemtaka waziri mwenye dhamana kuingilia kati suala hilo.
Akizungumza na mwanahabari hii Mwenyekiti wa Kumucha Group Donmillan Shirima amesema kuwa zoezi zima la ukiukwaji wa madai ya wachimbaji limegubikwa na harufu za rushwa ambapo wananchi wamekuwa wakikandamizwa bila kupewa haki yao ya msingi ambapo anayejiita mwekezaji amekuwa akipewa nafasi kubwa huku sheria ikipewa nafasi ndogo.
Amesema kuwa licha ya kufika kwenye mamlaka mbali mbali za serikali kisheria bado hawajapatiwa ufumbuzi kwani barua zao zimekuwa hazina majibu tokea mwezi watatu mwaka huu na wamefika hadi ofisi ya mkuu wa mkoa huo na kupeleka barua bila majibu yapata mwezi wa pili sasa huku mwenzao akibambikiwa kesi mbali mbali na wao kusimamishwa kazi kinyume na sheria.
“Unajua tunashangaa sana kwa jambo hili lililowazi kutopatiwa majibu ya kimsingi na yakisheria kwa sheria zipo wazi anayekutwa kwenye eneo na ameshaanza kazi na ameomba kisheria na kupimiwa anakuwa teyari kusubiria majibu ndani ya siku 28 lakini cha kushangaza miaka miwili imepita hadi mwaka huu mwezi wa tatu ndio tunaona mtu anakuja na kutuambia ana leseni tunashangazwa na hili tunaiomba serikali kulifuatilia hili tupewe haki zetu za msingi” alisema Shirima.
Alipotafutwa kwa njia ya simu kujibu madai ya wachimbaji hao Kamishna msaidizi wa madini Kanda ya Kati Sosthenes Masola amesema kuwa suala hilo amemuachia Afisa madini mkazi Silimu Tegalile kulishughulikia tokea mwezi wa Tano hadi sasa bila majibu na hata akipigiwa simu amekuwa hapokei jambo linalowawia vigumu kujua nini kinaendelea.
Nae Mkurugenzi wa Kondoa Minning Fei Kidee amesema kuwa wachimbaji hao kama wanamadai yeyote wamtafute kwani yeye hayupo teyari kuwatafuta wao kwani sehemu hiyo amepewa leseni na wizara ya madini hivyo haoni sababu ya kuketi au kuwaomba wachimbaji hao ila waondoke katika eneo hilo na kumuachia aanze kufanya kazi kwani ametumia gharama kubwa kulipata.
Juhudi zinaendelea kumtafua mkuu wa mkoa huo na mkuu wa wilaya hiyo kupata majibu ya madai ya wachimbaji hao ambao wamekuwa wakidai kudharauliwa ndani ya ofisi za serikali kwa kutitwa matapeli huku mwekezaji akidai yeye ni alwatani katika wizara ya madini na hakuna wa kumfanya kitu.
Hivyo makala WAMTAKA WAZIRI WA MADINI AIRUKI KUINGILIA KATI SUALA LAO
yaani makala yote WAMTAKA WAZIRI WA MADINI AIRUKI KUINGILIA KATI SUALA LAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAMTAKA WAZIRI WA MADINI AIRUKI KUINGILIA KATI SUALA LAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/10/wamtaka-waziri-wa-madini-airuki.html
0 Response to "WAMTAKA WAZIRI WA MADINI AIRUKI KUINGILIA KATI SUALA LAO"
Post a Comment