title : WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA
kiungo : WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA
WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA
Na Agness Francis,Globu ya jamii.
WASANII mbalimbali wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya Tamasha la Sport Music Festival ambalo linatarajia kufanyika leo Kanda ya Ziwa.
Lengo la tamasha hilo ni kuhakikisha wananchi wa Kanda ya Ziwa katika Sikuu ya Eid Elfitri wanasheherekea siku hiyo kwa kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.Tamasha hilo la aina yake litafanyika maeneo ya Geita,Mwanza na Kahama.
Kwa mujibu wa waandaaji wa tamasha hilo ni kwamba pia kutakuwa na michezo ya pikipiki pamoja na magari huku wakisindikizwa na wasanii mbalimbali wa Bongo fleva.Mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro Profesa Jay(Chadema)ambaye pia ni msanii wa kizazi kipya amewataka mashabiki zake wafike kumshuhudia akitoa burudani.
"Tangu niwe mbunge sijafanya shoo kubwa, hivyo hii ndio ya kwanza nitafanya maajabu kwenu,"amesema Prof. Jay.Kwa upande wa Snura Mushi a.k.a Snura amesema amejipanga kwa kufanya mazoezi licha ya kukaa mwezi mzima wa mfungo bila kufanya shoo. "Nimewaandalia vitu vingi na vipya mashabiki zangu,nimejipanga kutengeneza vitu vipya tofauti na mlivyovizoea,"amesema.
Wakati huohuo Msanii wa Bongo Fleva kutoka kundi la Weusi G Nako amewasili nchini ambako naye atashiriki katika tamasha hilo kwa kufanya shoo ya kibabe , hivyo amewataka mashabiki kjitokeza kwa wingi. Burudani hizo kwa siku ya leo zitaanzia Geita, kesho Mwanza na kumalizikia Kahama keshokutwa.
Mbunge wa jimbo la mikumi ambaye ni msanii wa kizazi kipya prifesa jay akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutua katika viwanja vya ndege jijini Mwanza,akizungumzia ujio wake mpya kwa wakazi wa kanda ya ziwa,ambapo amesema bado yupo fiti licha ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya shoo kubwa.
Msanii wa kizazi kipya kutoka weusi G Nako akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutua katika viwanja vya ndege jijini Mwanza kuhusu ujio wake tena kwa wakazi wakanda ga ziwa ambapo amewataka wajitokeze kwa wingi kushudia burudani ya uhakika kutoka kwake na shangwe zakutosha.
Mama wa chura snura mushi akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutua katika Viwanja vya ndege leo jijini mwanza ambapo amewataka mashabiki wa kanda ya ziwa wajitokeze kumshuhudia akitoa buruda yake ambayo itakua na vitu vingi vipya kwenye tamsha hilo la sport music festival litakalofanyika,Geita,Mwanza,Kahama katika kusheherekea sikukuu ya Iddy.
Hivyo makala WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA
yaani makala yote WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wasanii-kufanya-shoo-ya-kibabe-tamasha.html
0 Response to "WASANII KUFANYA SHOO YA KIBABE TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA"
Post a Comment