DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI

DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI
kiungo : DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI

soma pia


DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

NAIBU Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Faustine Ndugulile amesema hairuhusiwi katika duka la dawa kuwa na dirisha la ushauri kwani huo si utaratibu huku ikielezea sababu zinazosababisha usugu wa dawa.

Dk.Faustine Ndugulile amesema hayo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Famasi yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Akizungumzia maduka ya dawa kuwa na dirisha kwa ajili ya kutoa ushauri, Dk.Ndugulile amesema kisheria hairuhusiwi kwani kuna mgawawanyo wa majukumu.

"Kuna baadhi ya maduka ya kuuza dawa wameweke na madirisha kwa ajili ya kutoa ushauri.Hairuhusiwi na hivyo baraza la famasi linatakiwa kusimamia hili kwa kuhakikisha hakuna duka la dawa ambalo limeweka dirisha la ushauri,"amesema Dk.Ndugulile.

Akizungumzia usugu wa dawa kwa mtumiaji, Dk.Ndugulile amefafanua zipo sababu nyingi ikiwamo ya matumizi ya dawa yasiyo sahihi na ulaji holela wa dawa.Amefafanua mbali ya kuwapo kwa sababu hizo kuna tafiti ambayo imebaini kuna vimelea ambavyo ni sugu wa hali ya juu kwa dawa zote zilizopo duniani.

Wakati huohuo Dk.Ndugulile ameliezea baraza la Famasi kuwa anao ushahidi wa baadhi ya watalaam wa famasi si waaminifu kwani wamekuwa wakiiba dawa na hivyo hao wachache kuharibu sifa ya famasi.

Ameliomba baraza la famasi kuhakikisha wanachukua hatua dhidi ya wanaokiuka sheria za famasi kwani kukaa kimya kunatoa nafasi ya baadhi yao kukika sheria zilizopo, hivyo wafuatilie.Hivyo amesema wenye tabia hiyo ya kuiba dawa waache mara moja kwani Wizara yao inafuatilia huku akielezea kwa sasa hakuna tatizo la uhaba wa dawa kwani zipo za kutosha.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwakabidhi zawadi baadhi ya wadau wa Famasi kwa mchango wao katika sekta hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akionesha juu Bango Kitita la famasia baada ya kulizindua wakati  wa maadhimisho ya wiki ya Famasia yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. Kulia ni Msajili wa Baraza la Famasia Bi. Elizabeth Shekirego Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Bakari.



Hivyo makala DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI

yaani makala yote DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/dkndugulile-asema-hairuhusiwi-duka-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DK.NDUGULILE ASEMA HAIRUHUSIWI DUKA LA DAWA KUWA NA DIRISHA LA USHAURI"

Post a Comment