title : Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara
kiungo : Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara
Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara
Na MwandishiWetu
Wakulima wa ufuta nchini wametakiwa kuachanana kilimo cha mazoe and kufanya kilimo biashara. Hasa katika kuongeza tija ya uzalishaji ili kukabiliana na changamoto wakati bei inaposhuka pamoja na kuweka kumbukumbu na kuwasiliana na wanunuzi kabla ya kulima mazaoyao.
Hiyo ni pamoja na wakulima kujiunga katika vikundi rasmi au katika vyama vya ushirika ili kuweza kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha nchini ambapo serikali itawapatia dhamana kupitia vikundi hivyo.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba alisema hayo jijini Dar es Salaam katika kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilayaz a Bahi, Babati na Manyoni, kongamano hilo liliandaliwa na shirika la Farm Africa kwa kushirikiana na mashirika wenza ambayo ni INADES Tanzania, COSITA na MVIWATA.
“Mheshimiwa Rais Dkt John Magufuli mara kadhaa amekuwa akisisitiza umuhimu wa wakulima nchini kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kujikwamua kutoka kwenye kilimo kisicho na tija kwa sababu vyama vya ushirika vina fursa ya kupata dhama na ya serikali moja kwa moja,” alisisitiza.
Wadau wa walioshiriki kongamano hilo ni wakulima, wanunuzi wakubwa na wakati, halmashauri za Babati Manyara , Manyoni Singida, Bahi Dodoma na Kilwa, wakala wa mbegu ASA, wizara ya TAMISEMI, Viwanda na wadau wengine ni Shirika la TOSCI watoa huduma kwa njia ya tehama ambao ni wawakilishi kutoka mashirika ya Esoko na Sibesonke .
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen kushoto aliyesimama akifafanua jambo wakati wa wakati wa kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta kutoka wilaya za Kilwa, Bahi, Babati na Manyoni na liliandaliwa na shirika hilo, kulia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida Manyoni, Bw.Charles Fussi, wa pili kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki.
Meneja Mwandamizi wa Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki aliyeye simama akieleza jambo wakati wa kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilaya za Bahi, Babati, Kilwa na Manyoni lililoandaliwa na shirika hilo, kulia kwake mwenye laptop ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen na wengine ni wadau wa zao hilo.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt Charles Tizeba wa pili kulia akifafanua jambo wakati wa kongamano la siku mbili la wadau wa zao la ufuta nchini kutoka wilaya za Bahi, Babati na Manyoni na liliandaliwa na shirika la Farm Africa, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Farm Africa Bw. Ryan Whalen, kushoto Meneja Mwandamizi Program ya Kuendeleza Kilimo wa Shirika la Farm Africa, Bw Tumaini Elibariki na wa pili kushoto Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida Manyoni,Bw.Charles Fussi.
Wadau wa zao la ufuta kutoka wilaya za Kilwa, Bahi, Babati na Manyoni wakiwa katika kongamano la siku mbili la wadau wa zao hilo lililoandaliwa na shirika la Farm Africa.
Hivyo makala Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara
yaani makala yote Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wakulima-wa-ufuta-watakiwa-kufanya.html
0 Response to "Wakulima wa ufuta watakiwa kufanya kilimo biashara"
Post a Comment