WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO

WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO
kiungo : WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO

soma pia


WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WAKIMBIZI mkoani Kigoma wametakiwa kurejea nchini kwao, ili waanze kujishughulisha na masuala ya maendeleo kwani kwa sasa nchi zao ziko salama na amani imerejea.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala katika kambi ya Mtendeli wakati wa Siku ya Wakimbikiz Duniani.

Amesema sasa ni wakati wa wakimbizi waliko chini kurudi katika nchi zao kuendelea na majukumu mengine.Amefafanua mkapa sasa baadhi ya wakimbizi 6000 wamerejea nchini mwao kwa hiyari. "Wapo wengine bado wapo nchini kwetu kutokana na kushawishiwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi,"amesema.

Amewaambia wakimbizi hao ni vema wakarejea nchini kwao na kuendelea na maisha yao badala ya kubaki Tanzania kwasababu kuna watu wanawashawishi.Aidha amesema Serikali haitawavumilia wakimbizi wanaoishi katika kambi zilizopo wilayani hapo ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya kiualifu.

"Serikali imewahakikishia kuishi kwa amani na usalama wao pamoja na mali katika kambi yao na sambamba na kuilinda amani hiyo ambayo waliikuta nchini," amesema Ndagala Amefafanua kila mkimbizi anatakiwa kufata taratibu na sheria za nchi na kwa kila atakayekiuka taratibu hizo sheria haitamuacha salama lazima itafata mkondo wake.Pia amesema kuna changamoto ya uhalifu, kwani kuna baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakitoka kambini na kwekuharibu mazao katika mashamba ya watanzania.

Awali akisoma hotuba Mwenyekiti wa kambi hiyo Mtena Nizigiyumukiza ameiomba Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR), kufanya mahojiano na wakimbizi ambao hawako tayari kurudi nchini kwako ili wasikilizwe matatizo yao. "Tunaomba pia mtuongezee sabuni pamoja na chakula ikiwa sambamba na kubadilishiwa chakula kwani tumekuwa tukila ugali na imetufanya kutamani wali,"amesema Nizigiyumukiza.

Mkuu wa kambi hiyo Lulu Malima, amewataka wakimbizi hao kutunza mazingira ndani na nje ya kambi na kuacha tabia ya kukata miti ovyo.
Baadhi ya Wakimbizi wa kambi ya Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiadhimisha  katika siku ya wakimbizi duniani,
 Shughuli za burudani hapa na pale zilitolewa katika maadhimisho hayo hapo jana
 Baadhi ya Wakimbizi wa kambi ya Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiadhimisha  katika siku ya wakimbizi duniani,
 


Hivyo makala WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO

yaani makala yote WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wakimbizi-kigoma-wametakiwa-kurejea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO"

Post a Comment