title : WAKAZI MKOA WA PWANI WATAKIWA KULINDA MIRADI INAYOJENGWA
kiungo : WAKAZI MKOA WA PWANI WATAKIWA KULINDA MIRADI INAYOJENGWA
WAKAZI MKOA WA PWANI WATAKIWA KULINDA MIRADI INAYOJENGWA
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii
WAKAZI wa Rufiji mkoani Pwani wametakiwa kulinda miradi inayojengwa ili kupata wataalam wengi watakaoisaidia Serikali.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana baada ya kukagua majengo ya kisasa yaliyojengwa Kijiji cha Dohatul Khayr kupitia Taasisi ya Alat'a Chartable Foundation Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema mradi huo utasaidia kupata wataalamu mbalimbali.
"Mradi huu ni mkubwa kwa wilaya ya Rufiji utasaidia kupata wataalamu na wengi watakaoisaidia Serikali kwenye kazi mbalimbali za kimaendeleo," amesema Ulega.Ameongeza kuwa Wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti ziko nyuma kimaendeleo hivyo miradi inayoanzishwa itawawezesha kuhimiza maendeleo na kuzalisha wataalamu.
Mfadhili wa mradi huo kutoka Qata Nusser Al Khal amesema miradi huo ni miradi kwanza kwa Tanzania kujengwa kwa ufadhili ambapo umehusisha nyumba 32,kituo cha afya na msikiti.
"Miradi huu wa kwanza umegarimu Sh.bilioni 1.3 ambapo umehusisha nyumba ya ibada,hospital na nyumba 32 ambapo miradi utakaofuata utajenga majengo ya taaluma," amesema All Khal.
Kwa upande wa Shekh wa Wilaya ya Rufiji Othmani Kaporwa amesema kujengwa kwa miradi hiyo itawasaidi wakazi wa maeneo hayo.Wafadhili hao pia wanajenga mradi mkubwa katika jimbo la Mkuranga ambapo itakuwa na nyumba zaidi ya 30, shule ya msingi, sekondari na chuo cha ufundi.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Rufiji kwa niaba ya Waziri Mkuu katika hafla ya ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (alievaa koti) kwa niaba ya Waziri Mkuu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega akikagua bweni la kulala watoto yatima na wanaoIshi katika mazingira magumU kwa niaba ya Waziri Mkuu katika ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wa pili kulia alievaa koti akiwa pamoja na waumini wengine katika ibada ya Ijumaa katika msikiti uliopo ndani ya kijiji hicho.
Muomekano wa wa majengo pamoja yaliyopo katika kijiji cha Dohatl Khayr.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega akiwa ameambatana na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa kukagua majengo yaliyo jengwa katika kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.
Hivyo makala WAKAZI MKOA WA PWANI WATAKIWA KULINDA MIRADI INAYOJENGWA
yaani makala yote WAKAZI MKOA WA PWANI WATAKIWA KULINDA MIRADI INAYOJENGWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI MKOA WA PWANI WATAKIWA KULINDA MIRADI INAYOJENGWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/wakazi-mkoa-wa-pwani-watakiwa-kulinda.html
0 Response to "WAKAZI MKOA WA PWANI WATAKIWA KULINDA MIRADI INAYOJENGWA"
Post a Comment