ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA

ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA
kiungo : ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA

soma pia


ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA

 NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

ULE msemo wa kiswahili wa "mgeni njoo mwenyeji apone", unaweza kutumika kufatsiri neema ambayo taifa limepata kufuatia ziara ya siku mbili nchini ya Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, pichani juu.
Mhe. Mimica alianza ziara yake Novemba 2, kwa kutiliana saini makubaliano na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mjpango, ambapo EU imeahidi kutoa kiasi cha Euro milioni 50 ambazo zitatumika kupeleka umeme vijijini.
Serikali inapambana kuhakikisha vijiji elfu 12 (12,000) ambavyo bado havina umeme nchini vinapata huduma ya umeme ifikapo 2020.Kwa mujibub wa Afisa Habari wa EU hapa nchini Bi.Susanne Mbise, msaada huo wa Euro milioni 50 utasaidia kupeleka umeme kwenye vijiji 3,000.
Ziara ya Kamishna Mimica, ililenga kutembelea shughuli mbalimbali ambazo EU imekuwa ikifadhili,
Miongoni mwa maeneo ambayo Kamishna Mimica alitembelea ni pamoja na bandari ya Dar es Salaam, ambapo akiongea na uongozi wa bandari hiyo, Kamishna Mimica a,lieleza utayari wa EU katika kusaidia kub oresha bandari hiyo kwani ina msada mkubwa sio tu kwa Tanzania bali pia kwa nchi majirani.
Kamishna Mimica pia ametembelea kituo kinachosaidia vijana cha Nafasi Art Space kilichoko  Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo aliweza kusikiliza maoni yao na kujadiliana nao masuala mbalimbali yahusuyo changamoto za ajira na pia ukatili dhidi ya mtoto wa kike. "Kamishna Mimica amesema EU itatoa Euro  milioni 500 ili kusaidia kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto". amesema Bi. Mbise.
Kamishna huyo wa EU, alikutana na kujadiliana na makampuni makubwa ya kibinafsi ili kuona jinsi sekta binafsi inavyofanya shughuli zake hapa nchini na ziara hiyo ilimuwezesha pia kukutana na viongozi wa asasi za kiraia hapa nchini.
 Kamishna wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) anayeshughulikia mahusiano ya Kimataifa na Maendeleo, Mhe. Neven  Mimica, (kushoto), akiwa na balozi wa EU nchini, Mhe.Roeland van der Geer, wakati amkizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili nchini Novemba 3, 2017.(PICHA NA HABARI/K-VIS BLOG;Khalfan Said)
 Mhe. Mimica, akipokewa na Kaimu Mkurugezni Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, (TPA), Bw. Lazaro twange, alipotembelea bandari ya Dar es Salaam, Novemba 3, 2017. EU ni mdau mkubwa katika kjuisaidia TPA kuimarisha miundombinu yake.
 Mhe. Mimica akizun gumza na uongozi wa juu wa TPA.
 Mhe. Mimica akipeana mikono na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dotto James, baada ya kusaini makubaliano ambapo EU itatoa Euro milioni 50 kusaidia usambazaji umeme vijijini. Takriban vijiji 3,000 kote nchini vitafaidika na msaada huo. Serikali inapambana kuwafikishia umeme wana vijiji wa vijiji 12,000 a,mbavyo bado havijapata umeme na mpango huu umepangwa kukamilika 2020.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA

yaani makala yote ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/ziara-ya-kamishna-wa-eu-neven-mimica.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZIARA YA KAMISHNA WA EU NEVEN MIMICA YALETA NEEMA KWA TANZANIA"

Post a Comment