Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif.

Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif.
kiungo : Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif.

soma pia


Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Kamishna wa Biashara na Uwekezaji kutoka Nchini Australia Bibi Donna Massie, alipokuwa na mazungumzo yao yaliofanyika katika Ofisi yake katika jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar. 
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema upo uwezekano mkubwa wa Zanzibar kugeuka kuwa Dubai ya Afrika kutokana na juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Miundombinu tofauti.
Alisema Sekta ya Utalii hivi sasa inaendelea kushamiri katika kuliongezea mapato Taifa licha ya upande mwengine kupanua fursa za ajira hasa kwa Vijana   ambao wengi kati  yao wanaendesha maisha  kupitia sekta hiyo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Kamishna wa Biashara na Uwekezaji kutoka Nchini Australia Bibi Donna Massie  kwenye Ofisi yake ndogo iliyomo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema fursa zinazoendelea kutolewa katika masuala ya kukaribisha Uwekezaji Vitega Uchumi ndani na nje ya Nchi zinaifanya Zanzibar kuelekea katika uchumi imara unaoweza kupunguza utegemezi wa Nje.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimshauri Kamishna huyo wa Biashara na Uwekezaji Bibi Donna Massie kutoka Nchini Australia kuyashawishi Makampuni na Taasisi za Nchi hiyo kuzitumia fursa zilizopo Zanzibar katika kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi.
Alisema zipo Rasilmali nyingi kwenye Sekta ya Kilimo, Viwanda, Mawasiliano na hata Afya ambazo Makampuni na Taasisi za Nchi hizo zinaweza kuzitumia hata katika Mpango wa  Ubia katika kushirikiana na Taasisi za Kizalendo.
Balozi Seif alieleza kwamba Wataalamu wa Sekta ya Nishati  walipewa jukumu la kufanya utafiti wa upatikanaji wa Nishati Mbadala ya Umeme ili kuondokana na utegemezi wa mfumo mmoja tu wa upatikanaji wa huduma za Umeme kutoka Tanzania Bara.
Alisema ripoti za awali za utafiti huo uliogharamiwa na kusimamiwa na Umoja wa Ulaya {EU} zimeonyesha  uwezekano wa matumizi ya Umeme unaotokana na Nguvu za Jua pamoja na Upepo.
Hatuahiyo imechukuliwa na Serikali Kuu katika kuhakikisha kwamba changamoto zozote zitakazojitokeza katika miradi ya kiuchumi na ile ya Uwekezaji zisiweze kuteteresha  Miradi hiyo kutokana na hitilafu zinazoweza kujichomoza katika upatikanaji wa huduma za Umeme.
Naye kwa upande wake Kamishna wa Biashara na Uwekezaji kutoka Nchini Australia Bibi Donna Massie aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa umakini wake wa kuhakikisha Taifa linaelekea katika mfumo wa kuondokana na Mpango wa utegemezi katika Uchumi wake.
Hata hivyo Bibi Donna alitanabahisha kwamba Teknolojia mpya iliyopo hivi sasa inakuwa kwa haraka Duniani kiasi cha kuishauri Zanzibar iwe makini katika muelekeo wake wa kutaka kuingia katika Miradi mipya ya Mafuta na Gesi Asilia  hasa ikizingatia zaidi suala la Mazingira.
Kamishna wa Biashara na Uwekezaji kutoka Nchini Australia yupo Zanzibar kuangalia fursa ambazo Makampuni na Taasisi za Uwekezaji za Nchini mwake zinaweza kutumia nafasi hiyo kuwekeza Miradi yao Visiwani Zanzibar.


Hivyo makala Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif.

yaani makala yote Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/uwezekano-mkubwa-wa-zanzibar-kugeuka.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Uwezekano Mkubwa wa Zanzibar Kugeuka Kuwa Dubai ya Afrika Kutokana na Juhudi za Serikali ya SMZ. -Balozi Seif."

Post a Comment