JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA.

JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA.
kiungo : JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA.

soma pia


JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA.

Na  Bashir  Yakub. 

Kuna  mambo ambayo  yafaa  tujihadhari  nayo  sana  hasa  kipindi  hiki. Wengi wamefutiwa  umiliki wa  ardhi. Takwimu  za kufutiwa ni kubwa sana kipindi hiki kama ulikuwa hujui. Kwa  watu  wanaonunua  ardhi  na  kwenda  kuishi  nje  ya  nchi  hili  lawahusu  sana kabla hamjapoteza ardhi zenu.  

Najua  unachojua kuhusu  kutelekeza ardhi  ni pengine  kutokujenga,  au  kutoitumia  kama ilivyopangiwa matumizi, nk. Ni kweli lakini  hiyo ni maana  finyu  ya kutelekeza ardhi. Maana  ni  zaidi ya hiyo,  na  hapa tutaona  ili  ujihadhari na  uwezekano wa  kupoteza  ardhi  yako.

1.MAMBO  AMBAYO  UKIFANYA  UTAHESABIKA  KUTELEKEZA  ARDHI.

Mambo  haya  yameelezwa   na  Sheria  Namba  4  ya  ardhi  ya  1999 kifungu  cha  51(1).

( a ) Kutokulipa  kodi, tozo  au  ushuru  wowote  ambao  upo  kisheria  kwa  ajili  ya  ardhi  ni  kutelekeza  ardhi  kwa  mujibu  wa  sheria hiyo.  Mnazijua  kodi  za  majengo,  kodi  za  ardhi  nk.  Hizi  ni  muhimu  sana  na  kimsingi  ndizo  zinazoeleza  uhai  wa  ardhi  yako.

Ikiwa hulipi  hizi  hata  kama  eneo  hilo  umejenga  kiwanda  kinachofanya  kazi  saa  24  siku  7  za  wiki  bado  mbele  ya  macho  ya  sheria  unahesabika  kutelekeza  ardhi.  Dawa  ya  kuepuka  hili  ni  ndogo.  Lipa  hizo  kodi  na  tozo  kwa  mujibu  wa  sheria. Yamkini  hizi  huwa si  pesa  nyingi  sana ya  kumshinda  mmiliki  kulipa.

( b ) Jengo  ndani  ya  ardhi  kuwa  gofu  ni  kutelekeza  ardhi  kwa  mujibu  wa  sheria.  Lakini  pia   katika eneo  hilo  sheria  imetumia  neno “disrepair”.  Maana   yake  kutokufanya  ukarabati.  Kwa  tafsiri  hii  ni  kuwa  kumbe  hata  kutokufanyia  majengo  yetu ukarabati  nako ni  kutelekeza  ardhi. 

Utaona  katikati  ya  miji  yetu  majengo ya  zamani machafu,  yaliyopauka. Japo  ndani  mwake  watu  wanaishi  na  maofisi  yamo  bado kwa tafsiri  ya  neno  “disrepair”  ni  kuwa  jengo  hilo  limetelekezwa.  Na  sheria  imeeleza  zaidi  kuwa itakuwa  mbaya  zaidi  ikiwa  jengo  hilo  linahatarisha  afya  au maisha  ya  watumiaji  wake , majirani  au  hata  wapita  njia. 




                   KUSOMA  ZAIDI   



Hivyo makala JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA.

yaani makala yote JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/11/je-wajua-kutelekeza-ardhi-ni-pamoja-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JE WAJUA KUTELEKEZA ARDHI NI PAMOJA NA HAYA."

Post a Comment