title : MMILIKI WA IPTL ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA MKEWE MAHAKAMANI
kiungo : MMILIKI WA IPTL ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA MKEWE MAHAKAMANI
MMILIKI WA IPTL ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA MKEWE MAHAKAMANI
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth kuongea na mke wake mahakamani hapo baada ya kutukumuona kwa muda wa miezi mitatu.
Ruhusa hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi hilo kutokana na kutokuwa na kibali cha kumuona mumewe gerezani.
Kabla ya kutolewa kwa ruhusa hiyo, Wakili wa utetezi, John Chuma ameiomba mshtakiwa aweze kuonana na mkewe ambaye hajaweza kumuona kwa kipindi cha miaka mitatu sababu kipindi chote hicho alikuwa amefiwa na mama mkwe wake( mama wa mkewe).
"Mheshimia tunaomba mshtakiwa namba moja (Sethi) aweze kuzungumza na mke wake ikiwezekana hata kumkumbatia ili aweze kumpa pole ya kufiwa na mama yake kwa sababu bado hajapata kibali cha kuruhusiwa kwenda kumuona gerezani,"amesema.
Akijibu ombi hilo Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai, alidai, " kwa sababu ni ombi anaomba kusalimiana na mkewe hapa mahakamani sina pingamizi lakini kwa magereza kuna taratibu zake na mkewe alizivuruga yeye mwenyewe."
Kutokana na majibu hayo, Hakimu Shahidi aliruhusu mshtakiwa kuzungumza na mkewe mahakamani hapo chini ya uangalizi wa askari magereza.Kesi hiyo ambayo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, imeahirishwa hadi Julai 5, mwaka huu.
Mbali na Seth mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Rugemalira ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka kumi na mawili ya uhujumu uchumi ,utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni mia tatu.
Pichani kushoto ni mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth ambaye ameruhusiwa kuongea na mke wake mahakamani hapo baada ya kutokumuona kwa muda wa miezi mitatu.
Hivyo makala MMILIKI WA IPTL ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA MKEWE MAHAKAMANI
yaani makala yote MMILIKI WA IPTL ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA MKEWE MAHAKAMANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MMILIKI WA IPTL ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA MKEWE MAHAKAMANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/mmiliki-wa-iptl-aruhusiwa-kuzungumza-na.html
0 Response to "MMILIKI WA IPTL ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA MKEWE MAHAKAMANI"
Post a Comment