title : MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29
kiungo : MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29
MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itawasomea maelezo ya awali (PH) na kesi kuanza kuisikiliza kesi ya jinai inayowakabili viongozi wa juu wa tisa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kwa mfululizo kuanzia Juni 25 hadi 29 mwaka 2018.
Hati hiyo imekuja baada ya mawakili wa upande wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili Paul Kadushi, Wankyo Simon na Jackline Nyantori kuieleza mahakama kuwa, kesi ilikuja kwa ajili ya Ph .
Hata hivyo, Mahakama haikuweza kusoma PH kwa sababu mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Freeman Mbowe amefiwa na kaka yake na amesafiri jana kwenda kuzika Moshi.
Pia Mahakama imemtaka mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo, Mbunge wa Tarime mjini Estherher Matiko ambaye amekuwa akiripotiwa kuwa mgonjwa mara kadhaa, kuhudhuria mahakamani bila ya kukosa na asipofanya hivyo hatua dhidi yake zitachukuliwa.
Pia kesi hiyo imeshindwa kuendelea kusikilizwa ysikilizwaji wa PH leo sababu mawakili wanaowatetea washtakiwa hao Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya hawakuwepo walikuwa na kesi zingine, Kibatala ana kesi mahakama kuu. Huku Mtobesy alikuwa amehudhuria kesi Mahakama ya Afrika Mashariki Arusha na wamewakilishwa mahakamani hapo na mawakili Nashon Nkungu, Frederick Kihwelo na Hekima Mwesigwa.
Mbowe aliwakakilishwa mahakamani hapo na mdhamini wake Grayson Celestine ambaye aliwasilisha nakala ya cheti cha kifo mahakamani ili kuithibitishia mahakama, huku akiwasilishwa na mdhamini wake Patrick John ambaye alidai Matiko bado anaumwa na akawasilisha nyaraka ya mapumziko kutoka kituo cha afya ambayo inamapumziko ya siku saba kuanzia juni 21,2018 mpaka Juni 28,2018.
Hata hivyo nyaraka hiyo ilipingwa na Wakili Nchimbi kwa madai kuwa ni batili haina maelezo yanayojitosheleza ambayo yanaweza kuishawishi mahakama kuamini Matiko ni mgonjwa na anapaswa kupumzika kwa siku saba.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29
yaani makala yote MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/mahakama-kuwasomea-maelezo-ya-awali.html
0 Response to "MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29"
Post a Comment