title : KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA
kiungo : KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA
KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA
KAMPUNI ya Aon kupitia Minet imezindua rasmi JH Minet Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa safari iliyoanza 1998 ikiwa inatoa huduma za bima pamoja na mafao.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Minet Group Joe Onsando amesema kuwa kampuni hiyo mpya itakuwa chini Aon na hakuna kazi itakayopotezwa baada ya mabadiliko hayo.
Amesema kuwa Minet ni kampuni inayoaminika kote Afrika na nje ya bara hilo na wafanyakazi wa Aon ambayo sasa itajukulikana Minet katika nchi hizo na viongozi wao ambao wana ujuzi katika masuala ya viwanda wataendelea kuwa nafasi kama watendaji katika utoaji wa huduma.Onsando ameeleza kuwa mwaka 1997 kampuni hiyo ya JH Minet ilibadilishwa na kuwa Aon Minet na wanaendelea kujenga uchumi imara Afrika na itaendelea kuwa sehemu ya Aon katika utendaji kazi wao.
Onsando amefafanua kuwa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo hazitabadilika katika sekta zote kama vile kilimo, madini na mawasiliano.Pia amesema wanafurahishwa na namna uwekezaji unavyoendelea na kukua barani Afrika na wataendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao kwa sasa na baadaye.
Viongozi wa kampuni ya Minet wakizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa kufanya mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
Baadhi ya viongozi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya bima na mafao ya MINET wakisalimiana na baadhi wageni waalikwa waliofika kushuhudia mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
Baadhi ya viongozi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya bima na mafao ya MINET wakisalimiana na baadhi wageni waalikwa waliofika kushuhudia mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET wakifuatilia tukio hilo ambalo limefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
Mwanamuziki maarufu barani Afrika Vyone Chaka Chaka akisakata rumba na baadhi ya wageni waalikwa kwenye tukio la uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET.
Hivyo makala KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA
yaani makala yote KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/kampuni-ya-minet-group-yazindua-jh.html
0 Response to "KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA"
Post a Comment