title : KAMPUNI YA KANTON INVESTMENT, HALMASHAURI YA HANDENI WASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA ZAO LA MUHOGO
kiungo : KAMPUNI YA KANTON INVESTMENT, HALMASHAURI YA HANDENI WASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA ZAO LA MUHOGO
KAMPUNI YA KANTON INVESTMENT, HALMASHAURI YA HANDENI WASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA ZAO LA MUHOGO
HALMASHAURI ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga imewekeana saini na Kampuni ya Kanton Investment kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata zao la mihogo, ikiwa ni juhudi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuvutia wawekezaji nchini.
Ujenzi wa kiwanda hicho utakaogharimu Dola milioni 10 unatarajia kuchakata tani 200 za mihogo pamoja na kusafirisha tani 400,000 za wanga kutoka katika tani milioni 1.6 za mihogo mibichi itayosafirishwa nchini China.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki Wilayani Handeni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kanton Investment, John Rwehumbiza wakati wa hafla ya utiaji saini wa maktaba wa makubaliano hayo iliyohudhuriwa na viongozi wa Serikali.
Rwehumbiza amesema kampuni hiyo imeanza majaribio ya kununua na kusafirisha nje ya nchi zao la Muhogo na kuonesha kupendwa raia wa China, na hivyo kuahidi kufanya uwekezaji kwa kujenga kiwanda cha wanga na kununua mihogo ya wakulima na kuisafirisha nchini humo.
Aidha ameongeza kampuni yake pia imepanga kutoa elimu kwa wakulima wa zao la muhogo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wa zao hilo ambalo litawawezesha kutoa faida kubwa na hasa ukizingatia walaji wengi wa zao hilo wanatoka nje ya nchi ikiwepo China na Japan.
Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Mafukwe amesema Ofisi yake itahakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hao ili wafanye kazi katika mazingira wezeshi kama ilivyokusudiwa ili kuweza kuwanufaisha wakulima wa Wilaya hiyo.
Hivyo makala KAMPUNI YA KANTON INVESTMENT, HALMASHAURI YA HANDENI WASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA ZAO LA MUHOGO
yaani makala yote KAMPUNI YA KANTON INVESTMENT, HALMASHAURI YA HANDENI WASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA ZAO LA MUHOGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMPUNI YA KANTON INVESTMENT, HALMASHAURI YA HANDENI WASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA ZAO LA MUHOGO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/kampuni-ya-kanton-investment.html
0 Response to "KAMPUNI YA KANTON INVESTMENT, HALMASHAURI YA HANDENI WASAINI MAKUBALIANO KUENDELEZA ZAO LA MUHOGO"
Post a Comment