Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika

Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika
kiungo : Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika

soma pia


Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika

Takribani wateja 500,000 wanatembelea Jumia ndani ya mwezi katika mwaka huu 2018, kutoka wastani wa wateja 250,000 kwa mwezi mwaka 2017.Makampuni ya Kiafrika zaidi ya 60,000 na wafanyabiashara wamejiunga na Jumia. 

Ikiwa na dhamira ya kutengeneza mustakabali wa mazingira mazuri ya masoko na fursa za kuuza na kununua bidhaa pamoja na huduma za mtandaoni na kifedha, Jumia inaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya huduma za manunuzi ya mtandaoni barani Afrika.

Ikiwa imeanzishwa mwaka 2012, Jumia inajivunia kufanya kazi na makampuni zaidi ya 60,000 ya Afrika pamoja na wafanyabiashara wa kiafrika kwenye mtandao wake.

Akizungumzia juu ya shamrashamra za maadhimisho haya yakatakayodumu kuanzia Julai 2 mpaka Julai 15 mwaka 2018, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott amebainisha kuwa sherehe za mwaka huu zimekuja sambamba na sikukuu za Sabasaba hivyo kutoa fursa zaidi kwa wateja kununua bidhaa mbalimbali kwa gharama nafuu na ofa lukuki.

“Sabasaba ni maonyesho makubwa ya kibiashara siyo tu nchini Tanzania bali kwenye ukanda wa Afrika ya Mashariki kwa ujumla. Ni muhimu kwa wafanyabiashara na wateja ambapo hupata fursa ya kufanya maonyesho ya bidhaa na huduma tofauti, kuuza na kununua bidhaa mbalimbali. Kwa maneno mengine, Jumia ni kama maonyesho ya Sabasaba yanayofanyika kwa njiaya mtandao. 

Siku zote Jumia ina aina tofauti za bidhaa zinazopatikana kwa bei nafuu kabisa. Kwa hiyo sherehe za Jumia kwa mwaka huu itashiriki maonyesho ya Sabasaba, na kuwapatia wateja (watakaokuwepo Sabasaba na maeneo mengine) fursa ya kununua bidhaa kwa punguzo kubwa la bei, kujishindia zawadi, vocha za manunuzi na ofa kemkem kutoka mtandaoni na washirika wetu,” alisema Bw. Prescott.
  Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 6 ya Jumia barani Afrika na uzinduzi wa kampeni ya Sabasaba. Kulia ni wawakilishi kutoka kampuni ya simu ya FERO, ambao ni mojawapo ya washirika wa Jumia katika maonyesho ya Sabasaba mwaka 2018.

  Bw. Hemraj Bhardaraj, Meneja Ufundi wa kampuni ya simu ya FERO, akionesha mojawapo ya simu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) zitakazopatikana kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba katika banda  la Jumia. Wakifuatilia kwa umakini katikati ni muwakilishi mwenza kutoka FERO huku kushoto ni  Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James.
 Bw. Hemraj Bhardaraj, Meneja Ufundi wa kampuni ya simu ya FERO, akionEsha mojawapo ya simu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) zitakazopatikana kwenye viwanja vya maonyesho ya Sabasaba katika banda  la Jumia. Wakifuatilia kwa umakini kutoka kulia ni muwakilishi mwenza kutoka FERO huku akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko cha Jumia Tanzania, Bw. Albany James na Msimamizi wa Atsoko, Bi. Lisa Kameja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika

yaani makala yote Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/jumia-yaadhimisha-miaka-6-ya-mapinduzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jumia yaadhimisha miaka 6 ya mapinduzi ya biashara za mtandaoni Afrika"

Post a Comment