title : HELPAGE TANZANIA, JB GERIATRIC WATOA ELIMU YA AFYA KWA VIJIJI 10 KIBAHA
kiungo : HELPAGE TANZANIA, JB GERIATRIC WATOA ELIMU YA AFYA KWA VIJIJI 10 KIBAHA
HELPAGE TANZANIA, JB GERIATRIC WATOA ELIMU YA AFYA KWA VIJIJI 10 KIBAHA
VIJIJI 1O vya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ikiwemo cha Kongowe wamepatiwa elimu ya afya na vizazi rika pamoja na kupatiwa mafunzo mbalimbali kuhusu magonjwa yasiyo ambukiza.
Elimu na mafunzo hayo yametolewa na Shirika la HelpAge Tanzania kwa kushirikiana na asasi ya Jb Geriatric pamoja na HIV Center.
Mkurugenzi wa Asasi ya Jb Geriatric Judith Bagachwa amesema elimu na mafunzo hayo yametokana kupitia nguvu ya kijiji katika tekelezaji.Amesema lengo ni kuwawezesha wanakijiji kutumia rasilimali walizo nazo pasipo kutegemea kupata msaada wowote ule kutoka vyanzo vya nje.
"Mradi huu ulichaguliwa na wanakijiji wenyewe wa Kongowe ambao kwa busara zao waliona ni kitu ambacho kingeweza kunufaisha wanakijiji wote,"amesema. Pia ameongeza kwa muda mrefu toka mradi huo uanze Kongowe imekuwa ikisuasua hasa katika utekelezeji.
"Wanakijiji walikubaliana kuanzisha shamba la bustani ya kulima mbogamboga ili kuwasaidia wazee na pia watu mbalimbali kupata lishe bora,"amema.Pia wanakijiji walikubaliana kutoa elimu ya dawa ya kulevya ili kuwasaidia vijana ambao walionekana kuathirika na janga hilo.
Akieleza kwa undani kuhusu jitihada zilizofanyika Mzee Gadi Salumu Matitu amesema haikuwa rahisi kwani kila mtu alitegemea wangewezeshwa katika kuufanya mradi huu. "Wengi walisahau kuwa ilitupasa kutumia rasilimali tulizonazo ili kufanikisha mradi huu,"amesema.
Mmoja wa walioshiriki kutekeleza mradi huo Shaha Iddi amesema rasilimali waliyokuwa nayo ilikuwa nguvu tosha ya kufanikisha mradi wa kijiji ila watu wengi wamekuwa wakitaka kuwezeshwa kwanza ili kuweza kufanya kitu.Naye Mariam Ally anasema penye nia pana njia. Hiyo imejidhihirisha sasa kwani pamoja na changamoto zilizopo wamefanikiwa kufanikisha lengo lao.
Mshiriki mwingine katika mradi huu wa Kongowe Salma Hamadi Salum amesema mradi huo umekuwa wa manufaa kwao kama washiriki na hata pia jamii.
Mahindi kutoka shamba lo kongowe baada ya kuvunwa na sasa yanapikwa kwa ajili ya kuuzwa kwa wateja ambao ni wana kongowe.
Baadhi ya washiriki wa Mradi wa kijiji Kongowe
Hivyo makala HELPAGE TANZANIA, JB GERIATRIC WATOA ELIMU YA AFYA KWA VIJIJI 10 KIBAHA
yaani makala yote HELPAGE TANZANIA, JB GERIATRIC WATOA ELIMU YA AFYA KWA VIJIJI 10 KIBAHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HELPAGE TANZANIA, JB GERIATRIC WATOA ELIMU YA AFYA KWA VIJIJI 10 KIBAHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/helpage-tanzania-jb-geriatric-watoa.html
0 Response to "HELPAGE TANZANIA, JB GERIATRIC WATOA ELIMU YA AFYA KWA VIJIJI 10 KIBAHA"
Post a Comment