title : UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”
kiungo : UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”
UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem kwakushirikiana na Mkuu wa taasisi ya taaluma ya maendeleo Profesa Esta Dugumaro, Mkuu wa Mipango Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Pancras Bujuw wakikata utepe kuashiria umezindua wa kituo cha computer katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo Chuo Kikuu cha Dar es Salam.Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem (alieekaa) akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi huo.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo mara baada ya kuzindua kituo cha Kompyuta.
UBALOZI wa Kuwait nchini Tanzania umeanzisha mradi uitwao ““KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU” ambapo umezindua kituo cha Kompyuta katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo – Chuo Kikuu cha Dar es Salam. Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ambacho ni cha kwanza ilihudhuriwa na Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Ester Dugumaro, Mkuu wa Uwekezaji na Mipango wa UDSM Dr. Bujuluru pamoja na baadhi ya waalimu chuoni hapo.
Katika hotuba yake Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al-Najem alisisitiza kuwa Mradi Mpya unaolenga kuanzisha chumba cha Kompyuta katika taasisi za elimu ya juu ni muitikio wa wito uliotolewa na viongozi mbali mbali nchini kuhusiana na kuweka mkazo katika kuinua elimu na kuunga mkono juhudi za Raisi John Magufuli aliyetangaza kutoa elimu bure kwa wananchi wote.
Balozi Al-Najem aliongeza kuwa mradi huu una lengo la kuanzisha idadi kubwa zaidi ya vituo vya Kompyuta katika vyuo mbalimbali nchini kote kwa kushirikiana na Asasi na Jumuiya za misaada za Kuwait na Tanzania, na hii ni kutokana na umuhimu wa elimu kwa njia ya mtandao, Al-Najem aliongeza kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kitakua ndio kituo cha pili kufaidika na mradi huuu mkubwa, kikifuatiwa na chuo kikuu cha Zanzibar (SUZA).
Kwa upande wake Profesa Ester Dugumaro alitoa shukurani za dhati kwa Nchi ya kuwait kwa niaba ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa misaada mbali mbali inayotolewa kwa Tanzania katika sekta ya elimu, huku akielezea matumaini yake ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kuwait na vyuo vyengine nchini humo katika nyanja zote.
Bi. Dogomaro aliongeza kuwa wanafunzi wa Uzamili na Uzamifu ndio watakaofaidika zaidi na kituo cha kompyuta kilichoanzishwa na Ubalozi wa Kuwait ambapo wataweza kutumia mitandao kutafuta taarifa na maelezo kwa madhumuni ya utafiti.
Yafaa kuweka wazi kuwa Ubalozi wa Kuwaiti hapa Tanzania umeanzisha miradi mbalimbali katika kipindi cha hivi karibuni kama “Kisima cha Maji kwa Kila Shule” na “Maabara ya sayansi kwa kila shule” yenye lngo la kuisaidia Tanzania katika sekta ya elimu.
Hivyo makala UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”
yaani makala yote UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU” Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU” mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/ubalozi-wa-kuwait-waanzisha-mradi-kituo.html
0 Response to "UBALOZI WA KUWAIT WAANZISHA MRADI “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”"
Post a Comment