title : UPANDE WA MASHTAKA WAAMRIWA KUTOA MAJIBU UPELELEZI WA KESI YA VIGOGO WA UTHAMINI MADINI YA ALMASI SERIKALI
kiungo : UPANDE WA MASHTAKA WAAMRIWA KUTOA MAJIBU UPELELEZI WA KESI YA VIGOGO WA UTHAMINI MADINI YA ALMASI SERIKALI
UPANDE WA MASHTAKA WAAMRIWA KUTOA MAJIBU UPELELEZI WA KESI YA VIGOGO WA UTHAMINI MADINI YA ALMASI SERIKALI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili vigogo wawili wa uthamini wa madini ya Almasi wa Serikali kuwa hadi kufikia Mei 21 mwaka huu kuhakikisha wanatoa jibu kuhusu hatua ya upelelezi wa kesi hiyo ulipofikia.
Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbrad Mashauri baada ya Wakili wa Serikali, Saada Mohammed kudai mahakamani hapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba jalada lipo kwa DCI.
Kutokana na taarifa hiyo, Wakili wa utetezi Nickson Ludovick, amedai walitegemea upande wa mashtaka wangeiambia Mahakama ni lini wataendelea na kesi hiyo kwa sababu hapo awali walishasema upelelezi ulishakamilika.
Ameiomba Mahakama imwamuru (DPP) aseme lini kesi itaendelea kwa sababu katika kumbukumbu za mahakama zilizoko zinaonesha kesi ilishakuwa tayari kwa kuanza kusikilizwa.Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali Elia Athanas alidai jalada bado linashughulikiwa katika sehemu ambazo hazipo sawa na hakuna uzembe wowote unaofanywa na ofisi ya (DPP).
Baada ya kutolewa kwa hoja hizo, Hakimu Mashauri aliamuru upande wa mashtaka Mei 21, mwaka huu, kuja na majibu sahihi kuhusu hatua ya upelelezi ilipofikia. Washtkiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort) Archard Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu.
Katika kesi hiyo, washtakiwa hao ambao wanasota mahabusu kutokana na DPP kuzuia dhamana zao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia serikali hasara ya sh 2.4 bilioni.Kalugendo na Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini wanakabiliwa na shtaka la kuisababishia serikali hasara ya sh 2,486,397,982.54 ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.
Inadaiwa washtakiwa hao kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa Serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43 ambazo ni sawa na sh 2,486,397,9.
Hivyo makala UPANDE WA MASHTAKA WAAMRIWA KUTOA MAJIBU UPELELEZI WA KESI YA VIGOGO WA UTHAMINI MADINI YA ALMASI SERIKALI
yaani makala yote UPANDE WA MASHTAKA WAAMRIWA KUTOA MAJIBU UPELELEZI WA KESI YA VIGOGO WA UTHAMINI MADINI YA ALMASI SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UPANDE WA MASHTAKA WAAMRIWA KUTOA MAJIBU UPELELEZI WA KESI YA VIGOGO WA UTHAMINI MADINI YA ALMASI SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/upande-wa-mashtaka-waamriwa-kutoa.html
0 Response to "UPANDE WA MASHTAKA WAAMRIWA KUTOA MAJIBU UPELELEZI WA KESI YA VIGOGO WA UTHAMINI MADINI YA ALMASI SERIKALI"
Post a Comment