title : Leseni za madini kuanza kutolewa muda wowote
kiungo : Leseni za madini kuanza kutolewa muda wowote
Leseni za madini kuanza kutolewa muda wowote
Greyson Mwase na Asteria Muhozya, Morogoro
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema kuwa zoezi la utoaji wa leseni kwa ajili ya utafiti, uchimbaji na biashara ya madini linatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa mara baada ya uanzishwaji wa Tume ya Madini.
Profesa Msanjila ameyasema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari kwenye mkutano wa baraza la kwanza la wafanyakazi wa Wizara ya Madini mjini Morogoro tarehe 07 Mei, 2018 wenye lengo la kujadili utendaji kazi na namna ya kukabiliana na changamoto katika sekta ya madini.
Akielezea hatua iliyofikiwa ya zoezi hilo, Profesa Msanjila amesema kinachofanyika kwa sasa ni uchambuzi wa maombi ya leseni zote zilizokwishawasilishwa na kampuni mbalimbali zenye lengo la kujihusisha na shughuli za madini nchini.
Katika hatua nyingine, akielezea mkutano huo, Profesa Msanjila amesema mkutano huo wa kwanza unaambatana na uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi ambalo lipo kisheria.
Ameendelea kueleza kuwa masuala yatakayojadiliwa katika mkutano huo kuwa ni pamoja na umuhimu wa baraza la wafanyakazi, muundo wa Wizara ya Madini na maadili katika utumishi wa umma.
Ametaja masuala mengine kuwa ni pamoja na mapitio na utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018, mpango wa bajeti wa mwaka 2018/2019 na marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akisoma hotuba ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko kwenye mkutano wa baraza la kwanza la wafanyakazi wa Wizara ya Madini mjini Morogoro wenye lengo la kujadili utendaji kazi na namna ya kukabiliana na changamoto katika sekta ya madini.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akitoa ufafanuzi katika mkutano huo
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki (katikati waliokaa mbele), Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ( wa nne kutoka kulia waliokaa mbele), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini ( wa nne kutoka kushoto waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Leseni za madini kuanza kutolewa muda wowote
yaani makala yote Leseni za madini kuanza kutolewa muda wowote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Leseni za madini kuanza kutolewa muda wowote mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/leseni-za-madini-kuanza-kutolewa-muda.html
0 Response to "Leseni za madini kuanza kutolewa muda wowote"
Post a Comment