title : MUME AUAWA NA MKE KWA KUTAKA APIKIWE.
kiungo : MUME AUAWA NA MKE KWA KUTAKA APIKIWE.
MUME AUAWA NA MKE KWA KUTAKA APIKIWE.
Mtu mmoja aliyejulikana kwa Jina la Ahamad Salum mkazi wa Kata ya Namiyonga Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara ameuawa na Mke wake Sofia Swaleh Kwa Kuchomwa Kisu Kifuani kutokana na Majibizano ya Kupika Chakula Kingine.
Uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa kabla ya Mauaji hayo kulitokea Ugomvi baina ya Marehem na Mkewe ambapo Marehem alipikiwa Chakula na baada ya Kula Hakushiba hivyo akashinikiza Mke wake kumuandalia Chakula kingine Ndipo Ugomvi ukaibuka,na Ndipo Mke wa Marehemu Sofia Swalehe akachukua Kisu na Kumchoma eneo la Kifuani na kupelekea Ahamad Salum kufariki dunia kutokana na kupoteza Damu Nyingi.
Akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya amesema Watu wawili wanashikiliwa na Polisi Mmoja ni Jirani, Mussa Bakari ambaye aliingia ndani ya Nyumba baada ya kusikia Ugomvi ukiendelea na akashirikiana na Mke wa Marehem Sofia Swalehe kuua.
Aidha Kamanda Mkondya amewataka wananchi kutumia Viongozi wa Kiserikali na Kidini kuweza kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili katika Jamii.
'Nitoe rai kwa wananchii Magomvi hayana tija wajaribu kukaa na Kususuluhisha sio mnakaa na kugombana kwa kitu Kidogo mpaka mnapoteza Maisha kwa kitu Kidogo kama Chakula"
Hivyo makala MUME AUAWA NA MKE KWA KUTAKA APIKIWE.
yaani makala yote MUME AUAWA NA MKE KWA KUTAKA APIKIWE. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MUME AUAWA NA MKE KWA KUTAKA APIKIWE. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/mume-auawa-na-mke-kwa-kutaka-apikiwe.html
0 Response to "MUME AUAWA NA MKE KWA KUTAKA APIKIWE."
Post a Comment