title : VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI
kiungo : VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI
VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote.
Pia amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 27, 2018) wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma.
“Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo.”
Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zinazochochea maendeleo.
Akijibu ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Ofisini kwake jijini Dodoma, Aprili 27, 2018. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Maimuna Tarishi na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Shibuda
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Shibuda, katika kakao kati yake na kamati hiyo, ofisini kwake jijini Dodoma, Aprili 27, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Hivyo makala VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI
yaani makala yote VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/viongozi-wa-vyama-vya-siasa-watakiwa.html
0 Response to "VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI"
Post a Comment