title : TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA
kiungo : TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA
TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA
Na Mwandishi Maalum
Tanzania na Israel zimekubaliana kwamba , mataifa hayo mawili yana mengi ya kujifunza baina yao hususani katika eneo la utoaji wa haki na usimamiaji wa sheria.
Hayo yamejiri leo ( jumatatu) wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Sheria wa Israel Bi. Ayalet Shaked.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Jengo la Mikutano la Kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere ( JNICC), viongozi hao walikubaliana kwamba kuna haja na umuhimu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Israel kukutana kwa lengo la kuainisha maeneo ambayo Ofisi hizo mbili zinaweza kushirikiana.
“ Nadhani tuna mengi ya kujifunza kutoka kwenu na halikadhalika nanyi kuna maeneo ambayo mnaweza kujifunza kutoka kwetu. Hivyo basi, ninaamini kwamba pale itakapowezekana, kuna umuhimu wa mimi kukutana na mwenzangu ili tuweze kuangalia maeneo ya kipaumbele ambayo tunaweza kubadilishana uzoefu na kupanua wigo wa ushirikiano baina ya nchi zetu”, akasema Dk. Kilangi.
Akayataja maeneo ambayo anaamini Tanzania na Israel zinaweza kushirikiana ni pamoja na namna bora ya kuimarisha mifumo ya utoaji haki na ushauri wa kisheria wenye tija, pamoja na eneo la uwezeshwji ( capacity building).
Mwanasheria Mkuu , Dk. Kilangi ambaye alifuatana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw, Edson Athnas Makallo, aliyatumia mazungumzo kati yake na Waziri Shaked kuelezea baadhi ya majukumu yake anayoyatekeleza kama Mshauri Mkuu wa Serikali katika masuala yote yanayohusu sheria pamoja muundo mpya wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ambao umehusisha kuanzishwa kwa Wakili Mkuu wa Serikali.
Kwa upande wake, Waziri wa Sheria wa Israel, ambaye Tanzania inakuwa nchi yake ya kwanza kutembelea Barani Afrika, pamoja na kukubaliana na wazo la Dk. Kilangi la kuangalia uwezekano wa Wanasheria Wakuu kukutana katika muda utakaopangwa. Amesema kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni Ofisi nyeti na yenye hadhi ya juu kabisa katika nchi yoyote ile ikiwamo Israel.
Akaongeza kwamba, majukumu anayoyatekeleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi yanashabihiana na anayotekeleza Mwanasheria Mkuu wa Israel yakiwamo ya kuisimamia serikali katika masuala yote yanayohusu sheria, kuiwakilisha serikali katika mahakama za juu na mahakama za chini pamoja na kuendesha mashauri ya jinai hivyo wawili hao wakipata fursa ya kukutana bila shaka watakuwa na mengi ya kujadiliana na kushirikiana.
Waziri wa Sheria wa Israel Ayalet Shaked anaongoza ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Israel ambao upo hapa nchini kukutana na wafanyabiashara wa Tanzania.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akiwa katika mazugumzo na Waziri wa Sheria wa Israel Bi, Aylet Shaked. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimatifa wa Julius Nyerere ( JNICC) jijini Dar es Salaam, viongozi hao walikubaliana kwamba Tanzania na Israel zinayo maeneo ambayo kila nchi inaweza kujifunza kutoka kwa mwenzie hususani katika eneo la utoaji haki na usimamiaji wa sheria na kwamba kuna haja kupitia kwa Wanasheria Wakuu wa Serikali wa nchi hizo mbili kukutana ili kujadiliana maeneo ya kushirikiana. Waziri wa Sheria wa Israel yupo nchini akiongoza ujumbe wa wafanyabiashara.
Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi amekutana na kufanya mazugumzo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Said Hassan Said. Katika mazungumzo yao viongozi hao wamebadilishana mawazo ya namna ya kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku yanayosimamia masuala ya sheria na utaoaji haki. Pichani Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bw. Said Hassan Said akimkabidhi Dk. Adelardus Kilangi Katiba ya Zanzibar ( picha na Ofisi ya AG
Hivyo makala TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA
yaani makala yote TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/tanzania-na-israel-kuangalia-namna-ya.html
0 Response to "TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA"
Post a Comment