title : TAARIFA YA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO
kiungo : TAARIFA YA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO
TAARIFA YA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600 |
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM,
Tanzania.
|
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za mafunzo ya muda mrefu kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Pan African (PAU).
Mafunzo hayo ambayo yapo kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu yatatolewa katika kozi mbalimbali zikiwemo Baiolojia, Hesabu, Uhandisi, Sayansi ya Afya, Usimamizi wa Mazingira, Sayansi ya Michezo, Mifugo, Uongozi na Mtangamano, Lugha, Ukalimani wa Mikutano na Ufasiri, Uhandisi wa Maji na Nishati.
Kwa waombaji wa Shahada ya Uzamili wanatakiwa kuwa na miaka isiyozidi 30 kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 35 kwa waombaji wanawake. Aidha, kwa waombaji wa Shahada ya Uzamivu wasiwe na miaka zaidi ya 35 kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 40 kwa waombaji wanawake.
Maombi ya mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao (online) kupitia anuani ya barua pepe ya pau-au.net. Mwisho wa kutuma maombi ya fursa hizi ni tarehe 20 Aprili, 2018. Maelezo ya ziada kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia pau.scholarships@africa-union.org au www.pau-au.net. Mratibu wa Mafunzo haya ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Hivyo makala TAARIFA YA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO
yaani makala yote TAARIFA YA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA YA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/taarifa-ya-fursa-za-ufadhili-wa-masomo.html
0 Response to "TAARIFA YA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO"
Post a Comment