title : SHIRIKA LA PATHFINDER LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA THAMANI YA MILIONI 19
kiungo : SHIRIKA LA PATHFINDER LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA THAMANI YA MILIONI 19
SHIRIKA LA PATHFINDER LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA THAMANI YA MILIONI 19
Meneja mradi wa shirika la PATHFINDER Amgelo Kihaga akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Monduli, Idd Hassan Kimanta vifaa tiba ikiwa ni kitanda cha upasuaji (OPERATING BED) chenye thamani ya milioni 19,mikasi na nyembe ,Shirika hilo la Parthfinder la kimataifa lililo sajiliwa hapa nchini Tanzania linalofadhiliwa na shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID)inatekeleza miradi mbalimbali kwa miaka mitano shirika hilo linafanya kazi katika hifadhi za Taifa (TARANGIRE NATIONAL PARK ECOSYSTEM) Kwa lengo la mradi wa watu,afya,mazingira,uzazi wa mpango,cocoba na boma za mfano.
Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Hassan Kimanta akitoa shukrani mara baada ya kupokea vifaa tiba ikiwa ni kitanda cha upasuaji (OPERATING BED) chenye thamani ya milioni 19 kutoka katika shirika la Parthfinder.
Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha
SHIRIKA la Parthfinder la kimataifa lililo sajiliwa hapa nchini Tanzania linalofadhiliwa na shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID) limekabidhi vifaa tiba vyenye dhamani shilingi milioni 19,000,000 katika vituo vya afya vya wilayani Monduli.
Akikabidhi vifaa hivyo meneja mradi wa shirika hilo Angelo Kihaga amesema kuwa shirika lao linatekeleza miradi mbalimbali kwa miaka mitano pia wanafanya kazi katika hifadhi za Taifa za TARANGIRE NATIONAL PARK ECOSYSTEM na mradi wao unalengo la kusaidi sekta mbalilimbali ikiwa ni pamoja na kusaidia watu,afya,mazingira,uzazi wa mpango,cocoba na boma za mfano.
Amesema msaada huu ni moja lengo lililopo katika mradi wao wa miaka mitano ambao shirika linatekeleza ambapo alitaja baadhi ya vitu ambavyo wamevitoa kuwa ni kitanda kwa ajili ya mama kujifungulia,mikasi,sindano ,glops pamoja na vifaa tiba vingine mbalimbali.
Kihanga amesema kuwa mradi wao wamelenga kufikia mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Arusha pamoja na Mkoa wa Manyara pia watalenga zaidi kusaidia watu katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya pamoja na Mazingira.
Akizungumza mara baada yakupokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta amelishukuru shirika hilo kwa kuwa mdau mkubwa wa shughuli za maendeleo wilayani Monduli na kuwahaidi kuwa atavisimamia vyema na kuvitunza ili kuweza kuendelea kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo hususa ni wamama wanaoenda kujifungua.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amelitaka shirika pamoja na mashirika mengine kuendela kutoa misaada mbalimbali hususani katika sekta ya afya kwa ajili ya vituo vya afya vya wilaya hiyo ya monduli.
Shirika hilo natekeleza miradi mbalimbali kwa miaka mitano shirika hilo linafanya kazi katika hifadhi za Taifa (TARANGIRE NATIONAL PARK ECOSYSTEM) Kwa lengo la mradi wa watu,afya,mazingira,uzazi wa mpango,cocoba na boma za mfano.
Hivyo makala SHIRIKA LA PATHFINDER LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA THAMANI YA MILIONI 19
yaani makala yote SHIRIKA LA PATHFINDER LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA THAMANI YA MILIONI 19 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHIRIKA LA PATHFINDER LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA THAMANI YA MILIONI 19 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/shirika-la-pathfinder-latoa-msaada-wa.html
0 Response to "SHIRIKA LA PATHFINDER LATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA THAMANI YA MILIONI 19"
Post a Comment