MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA

MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA
kiungo : MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA

soma pia


MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
KATIBU Mkuu UWT Taifa, Mwalimu Queen Mlozi ,ameutaka umoja huo wilaya na mikoa ,kujiwekea mikakati ya kumkomboa mwanamke kisiasa ,kiuchumi na kijamii pamoja na kuwasemea wanyonge ili kujiinua kimaisha.

Aidha, amewataka wanawake ,washikamane kwa kujenga mahusiano mema kwa lengo la kuimarisha umoja huo .

Pamoja na hayo ,wajitume kwa kuanzisha miradi ya kujikwamua kiuchumi ili waweze kujitegemea na kuondokana na hali ya kuwa ombaomba kwenye familia .

Alitoa rai hiyo ,wakati akizungumza na kamati ya utekelezaji na wanachama wa UWT Mkoa wa Pwani ,katika ofisi za CCM Mkoani humo .

Aliwasihi ,viongozi wa umoja huo ,kurudi katika katiba ya UWT ambavyo inaelekeza kuwajengea uwezo wanawake katika kuwakomboa kimaisha.

"Ninawaomba wanawake tupendane ,wanasema adui ya mwanamke ni mwanamke lakini mimi siamini hilo,tushauriane tusonge mbele wanawake ni jeshi kubwa ,kwanza kwa kumsemea mh .Rais Dk.John Magufuli kwa kueleza mazuri yanayofanywa na serikali yetu "

"Pili tuwasemee na wanawake wenzetu walio wanyonge,wanapokuwa na shida tuseme sisi tukemee ili tusonge mbele " 

Mwalimu Queen alieleza ,hakuna kitu kikubwa dunia kama mtaji wa mahusiano mazuri na wengine ,hivyo ni lazima wapendane.

"Weka pembeni mali, weka pembeni pesa lakini tujenge mahusiano baina yetu" alisema Mwalimu Queen.

Mwalimu Queen aliwaomba ,kuendelea kuongeza idadi ya wanachama ndani ya jumuiya kuanzia ngazi za chini  na kulipia kadi kwani ndio mtaji wa kisiasa .

Nae mwenyekiti wa UWT Mkoani Pwani ,Farida Mgomi aliwasihi wanawake kujishughulisha na kujiunga vikundi ili kujikomboa kimaisha na kuondokana na utegemezi .

Alisema kuwa ,kwasasa wanajenga Pwani mpya ,CCM mpya na UWT mpya hivyo umoja na mshikamano ndio nguzo pekee kwao.

Farida aliahidi kwa niaba ya UWT mkoani hapo, kuyafanyia kazi maagizo waliyopatiwa kwa hali na mali kwa kuzingatia kwamba umoja huo ni chachu ya maendeleo kwa Taifa .

Awali Katibu Mkuu UWT Taifa na Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ,walichukua muda mchache wa kuzungumza na kamati hiyo kwa siri ikiwa ni sehemu ya kukumbushana majukumu yao katika utekelezaji wa ilani ya CCM na kusimamia kundi la wanawake .
 Katibu wa UWT Taifa ,Mwalimu Queen Mlozi (katikati)akizungumza na wanawake na wanachama wa UWT Mkoani Pwani. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
 Mwenyekiti wa UWT Mkoani Pwani ,Farida Mgomi ( mwenye kipaza sauti) akizungumza na akinamama wa umoja huo nje ya ofisi ya CCM mkoa ,wakati katibu wa UWT Taifa ,Mwalimu Queen Mlozi (wa kulia )alipokwenda kuzungumza na kamati ya utekelezaji ya UWT Mkoani Pwani, .(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Katibu wa UWT Taifa ,Mwalimu Queen Mlozi (wa kulia )akizungumza jambo baada ya kumsimamisha Mwenyekiti wa UWT Mkoani Pwani ,Farida Mgomi ( wa kushoto) katika kikao cha kamati ya utekelezaji ya UWT Mkoani Pwani, ambapo katibu huyo alipata nafasi ya kuwaelekeza na kuwakumbusha machache kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kikazi wakati tukielekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi Mkuu 2020.


Hivyo makala MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA

yaani makala yote MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/mwalimu-queenaitaka-uwt-kuyasemea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWALIMU QUEEN,AITAKA UWT KUYASEMEA MATATIZO YA WANYONGE ILI KUWAKOMBOA KIMAISHA"

Post a Comment