Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu

Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu
kiungo : Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu

soma pia


Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Juma Assad amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli inaendelea vizuri na uwekaji wa mahesabu uliopelekea kupungua kwa hati chafu katika Taasisi na miradi mbalimbali ya Serikali. 

Prof. Assad ameyasema hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2017.

"Katika ukaguzi wa hesabu nilioufanya katika Serikali Kuu na Taasisi zake, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2016/17 nimetoa jumla ya Hati 561 za ukaguzi. Kati ya hati hizo, Hati zinazoridhisha ni 502 sawa na asilimia 90, Hati zenye shaka ni 45 sawa na asilimia 90, Hati zenye shaka ni 45 sawa na asilimia 8, Hati zisizoridhisha ni Saba sawa na asilimia Moja na Hati Mbaya ni Saba sawa na asilimia Moja," alisema Prof. Assad. 

Amesema, katika ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Taasisi mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ametoa jumla ya Hati za Ukaguzi 742 ambapo Hati zinazoridhisha ni 697 sawa na asilimia 94, Hati zenye shaka ni 44 sawa na asilimia 5.9 na Hati isiyoridhisha ni moja, Hati hii imetolewa kwa mradi wa maji (WSDP) unaotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ya Wilaya ya Makete. 

Naye, Mjumbe wa Kamati ya LAAC Mhe. Abdallah Mtolea amezipongeza Halmashauri zilizofanya vizuri kwa kuonekana kupunguza idadi ya hati chafu na kushamiri kwa hati safi.

Aidha Mhe. Mtolea amesema kuwa kamati hiyo itaziita Halmaushari na kufanya nazo mahojiano bila kuujali matokeo ya ukaguzi kama zilifanya vizuri au vibaya ili kuhakikisha kuna kuwa matumizi mazuri ya fedha za umma.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Juma Assad akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu  ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2017.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC, Naghenjwa Kaboyoka akizungumza kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali baada ya CAG kuwasilisha ripoti za Hesabu za Serikali  kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2017.
 Sehemu ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Juma Assad  leo mjini Dodoma kuhusu ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2017.
Mbunge wa Temeke, Abdalah Mtolea akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya LAAC mara baada ya  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Juma Assad kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ripoti za Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia June 30, 2017.Katikati ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Juma Assad na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC mhe. Naghenjwa Kaboyoka.(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)


Hivyo makala Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu

yaani makala yote Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/serikali-yapunguza-idadi-ya-hati-chafu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Serikali Yapunguza Idadi Ya Hati Chafu"

Post a Comment