RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA

RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA
kiungo : RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA

soma pia


RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi kabla ya kuzindua rasmi Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipigiwa makofi mara baada ya kumaliza kusoma hotuba yake na kuizindua rasmi Taasisi hiyo isiyo ya Kiserikali ya Jakaya Mrisho Kikwete(JMKF) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kabla ya uzinduzi wa Taasisi hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya (JKMF) Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuizindua. PICHA NA IKULU

*Azungumzia mambo makubwa ambayo aliyafanya kwenye utawala wake ambayo yatakumbukwa
*Azindua rasmi Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation,aahdi Serikali kutoa ushirikiano mkubwa
*Alezea Kikwete alivyosababisha awe Rais wa Awamu ya Tano, Kikwete azungumzia malengo ya taasisi

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii.

RAIS Dk. John Magufuli amesema kwa kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye uongozi wake kuna mambo makubwa ya maendeleo katika nchi yetu huku akitanguliza uzalendo mkubwa Watanzania wanamkumbuka na wataendelea kukumbuka watake wasitake.

Pia ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake za dhati kwa Rais mstaafu Kikwete kwani ndio amesababisha awe Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano huku akitumia nafasi hiyo kuahidi kuwa atahakikisha Serikali yake itashirikana na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete inayofahamika kwa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)ambayo ameizindua rasmi leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

"Mzee wangu Kikwete naomba niseme kutoka moyoni wakati wa uongozi wako umefanya mambo makubwa ya kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzanania.Kuna miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ameifanya na imeacha alama ambayo itatufanya watanzania tumkumbuke.Kwa kazi ambayo umeifanya kwa uzalendo mkubwa ndani ya nchi yetu Watanzania tunakukumbuka na tutaendelea kukumbuka watake wasitake,"amesema Rais Dk.Magufuli.

Ametaja ipo mifano mingi hai ya mambo ambayo ameyafanya Rais mstaafu Kikwete kwenye Serikali ya Awamu ya nne na baadhi ya miradi hiyo lipo  la ujenzi wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya barabara nchi nzima, ujenzi wa miradi ya maji , umeme na kuimarisha sekta muhimu za afya, kilimo na vijana.

"Rais mstaafu Kikwete alilitumikia Taifa la Tanzania kwa uadilifu mkubwa.Tabia ya binadamu wamekuwa na kawaida ya kumsifu mtu baada ya kufa na kusema pengo halitazibika wakati si kweli kwani kama ni nafasi ya uongozi inaweza kujazwa wakati huohuo.Kwa Rais mstaafu na mzee wangu Kikwete naomba nikusifu ukiwa hai tena upo mbele yangu unatabasamu.Umefanya kazi kubwa ya kizalendo kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzania na unastahili sifa na shukrani kutokana na mchango wao wa kuleta maendeleo kwenye nafasi mbalimbali.

"Ulipokuwa Rais wa Tanzania umefanya mambo makubwa zaidi kwa ajili ya nchi yetu. Katika utawala wako umefanikisha ujenzi wa shule za sekondari za kata , ujenzi wa Hospitali ya Mloganzila na miradi mingine mikubwa ambayo umeifanya na sote ni mashahidi kwa yale ambayo umeyafanya,"amesisitiza Rais Dk.Magufuli na kuongeza mbali ya kuwa Rais mzee Kikwete ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Bara la Afrika na nchi za ulaya na Dunia kwa ujumla na kote huko ametoa mchango mkubwa wa kuleta maendeleo .

Rais Magufuli amesema uzalendo wa mzee Kikwete kwa nchi yake umemfanya hata baada ya kustaafu kuamua kuanzisha taasisi ambayo leo amezindua rasmi na vipaumbele vya taasisi hiyo havina tofauti na vile ambavyo anavitekeleza kwenye Serikali yake , hivyo ameahidi kumpa ushirikiana mkubwa kufanikisha malengo hayo na kuomba wadau wengine wakiwamo mabalozi nao kuunga mkono kazi za taasisi hiyo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


Hivyo makala RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA

yaani makala yote RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/rais-magufuli-mzee-kikwete-watanzania.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAIS MAGUFULI: MZEE KIKWETE WATANZANIA TUNAKUKUMBUKA"

Post a Comment