title : RC MAKONDA AAHIDI KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WOTE WALIOTELEKEZWA
kiungo : RC MAKONDA AAHIDI KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WOTE WALIOTELEKEZWA
RC MAKONDA AAHIDI KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WOTE WALIOTELEKEZWA
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema watoto wote ambao wametelekezwa na baba zao ambao wamefika kwenye ofisi yake na mama zao ili kupata msaada wa kisheria atahakikisha anawakatia bima ya afya ili kusaidia wapate matibabu bure.
Makonda ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na wanawake ambao wamezalishwa na kisha kutelekezwa na waume zao ambao wamefika kwake kupata msaada wa kisheria ambapo ameelezea kuwa wale wote waliofika kwake basi watoto wao watakatiwa bima ya afya.
Amesema anatambua changamoto ambazo akina mama hao wanazipitia na kuelezea kuwa kutokana na jitihada zake za kuwasaidia ametoa mdau ambaye ameahidi kumsaidia katika kuhakikisha watoto hao wanapata bima ya afya ambayo itawawezesha kupata huduma za afya pindi wanapougua.
"Mungu anatenda miujiza yake, kuna mtu mmoja ameona kazi nayoifanya ya kusaidia mama hawa,basi akajitolea kuwa atakata bima kwa ajili ya watoto wote ambao wamefika hapa na mama zao kwa ajili ya kupata msaada.Hivyo niwaambie wote mliopo hapa watoto wenu tutaeakatia bima ya afya ili wapate huduma za matibabu bure,"amesema Makonda hali iliyoibua shangwe kutoka kwa akina mama hao ambapo wapo waliozimia kutokana na habari hiy njema kwao.
Wakati huohuo Makonda amesema kuwa mpaka sasa watu mashughuli walitelekeza watoto wao wamefikia 107.
Makonda amesema idadi hiyo imebainika jana na juzi wakati wa mchakato huo ambapo pia amesema si kundi hilo tu la watu mashughuli kuna kundi la watu ambao wanaona aibu kufika katika eneo hilo.
"Hawa watu wanaona aibu kufika ofisini ofisini hapa, hakuna kukutana na mimi chemba, habari yakupigiana simu kuniambia Mheshimiwa naomba nije peke yangu hakuna", amesisitiza Makonda
"Watu Mashughuli, watu wenye heshima tukikupima DNA nakugundua mtoto ni wako, basi utalipa fidia zote za huyo mtoto".
Amesema wale wanaokaidi wito kufika ofisini hapo, kuanzia kesho watapelekewa barua pamoja na kupigiwa simu.
Zoezi hilo lakubaini Wazazi waliokimbia watoto wao lilianza siku ya Jumatatu ya April 9, 2018 na linatarajiwa kumalizika siku ya Ijumaa April 13 mwaka huu.
Baadhi ya Akina Mama waliojitokeza katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kudai fidia za Watoto wao kwa Wazazi wenzao waliokimbia watoto hao.
Mmoja wa Maafisa wa Ustawi wa Jamii akiwasikiliza Wazazi wa Kiume walioitikia wito kufika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya akina Baba waliotikia wito kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusikiliza malalamiko kwa wake zao. (PICHA NA EMMANUEL MASSAKA)
Hivyo makala RC MAKONDA AAHIDI KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WOTE WALIOTELEKEZWA
yaani makala yote RC MAKONDA AAHIDI KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WOTE WALIOTELEKEZWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AAHIDI KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WOTE WALIOTELEKEZWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/rc-makonda-aahidi-kuwakatia-bima-ya.html
0 Response to "RC MAKONDA AAHIDI KUWAKATIA BIMA YA AFYA WATOTO WOTE WALIOTELEKEZWA"
Post a Comment