title : MITI YA ASILI IPANDWE NA KUTUNZWA KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO-LUAMBA
kiungo : MITI YA ASILI IPANDWE NA KUTUNZWA KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO-LUAMBA
MITI YA ASILI IPANDWE NA KUTUNZWA KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO-LUAMBA
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
JAMII imehimizwa kupanda miti hasa ya asili ambayo ipo hatarini kutoweka pamoja na kulinda mazingira kwa faida na manufaa ya kizazi kijacho.
Aidha wananchi wameaswa kuacha kukata miti na misitu ovyo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha kuondoa uoto wa asili.
Rai hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la – SAHO-linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti na kuhimiza kutunza mazingira , Emmanuel Luamba wakati wa uzinduzi wao wa kampeni ya upandaji miti kata ya Visiga ,Kibaha Mkoani Pwani.
Alisema wananchi wanahimizwa kupanda miti lakini isisahaulike miti ya asili ikiwemo mninga,mkwaju,mkongo ambayo ina faida zake katika kukuza uchumi ,kuleta hewa safi na kuwa na nchi ya kijani.
Luamba alieleza wameotesha miche ya miti ya asili ipatayo 10,000 ambayo wanaisambaza iweze kupandwa taasisi za umma ikiwemo mashuleni ,kwa wananchi kata ya Visiga, kisha ngazi ya halmashauri na baadae Mkoa.
“Tumeanzia taasisi za umma ikiwemo shule mbalimbali na jamii ili kuwa na uelewa wa kujua faida za miti hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vinavyokuja” alielezea Luamba.Akizungumzia ujio wa shirika hilo ,mwenyekiti huyo alibainisha wanatarajia kuwa na matawi nchi nzima .
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake baada ya kupanda moja ya mche wa mti wa asili ,katika shule ya msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili inayofanywa na shirika hilo
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Fokas Bundala(wa kushoto) akipanda mche wa mti wa asili aina ya mninga ,katika shule ya msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili inayofanywa na shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kulia) ni diwani kata ya Visiga Mbegu Kambi Legeza.Picha na Mwamvua Mwinyi.
Hivyo makala MITI YA ASILI IPANDWE NA KUTUNZWA KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO-LUAMBA
yaani makala yote MITI YA ASILI IPANDWE NA KUTUNZWA KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO-LUAMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MITI YA ASILI IPANDWE NA KUTUNZWA KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO-LUAMBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/miti-ya-asili-ipandwe-na-kutunzwa-kwa.html
0 Response to "MITI YA ASILI IPANDWE NA KUTUNZWA KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO-LUAMBA"
Post a Comment