title : MBUNGE CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO
kiungo : MBUNGE CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO
MBUNGE CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO
Mbunge wa Tarime Vijijini, kupitia tiketi ya Chama cha Maendeleo Chadema, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu kujibu mashtaka ya kufanyaka mkusanyiko/maandamano yasiyo halali yenye vurugu na uchochezi wa chuki kinyume na sheria.
Heche anafanya jumla ya viongozi wa Chadema wanaoshtakiwa mahakamani hapo kwa makosa kama hayo ni kufikia nane ambao ni Washtakiwa hao ni Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu,Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika,Mbunge wa Tarime mjini Ester Matiko na Katibu wa chama hicho Dk Vicenti Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.
Akisomewa hati ya mashtaka na wakili wa Serikali Mwandamizi Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri imedaiwa, Februari 16,2018, katika barabara ya Kawawa Mkwajuni wilayani Kinondoni Dar es Salaam.
Mshtakiwa akiwa na vingozi wenzake hao walikusanyika kutekeleza lengo la pamoja waliendelea katika mkusanyiko huo na kufanya watu waogope kwamba watakwenda kusababisha uvunjifu wa amani.
Pia wanadaiwa February 16, 2018 katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni Dar es Salaam, wakiwa wamekusanyika wao na wenzao 12 ambao hawajafikishwa mahakamani, wakiwa kwenye maandamano na pasipo kuzingatia agizo lililotolewa na afisa polisi Gerald Ngiichi waligoma na kuendelea na maandamano na kusababisha kifo cha Aquilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi waliumia kutokana na mkusanyiko huo.
Aidha Heche anadaiwa kuwa, siku hiyo katika viwanja vya Buibui vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam akiwa anahutubia wananchi na wakazi wa eneo hilo katika mkutano wa Hadhara alitoa matamshi ambayo yalielekea kuleta chuki na manung'uniko miongoni mwa wananchi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Hata hivyo mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana. Na kesi imeahirishwa hadi Aprili 16 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya washtakiwa wote kusomewa Maelezo ya awali.
Mbunge wa Tarime Vijijini, kupitia tiketi ya Chama cha Maendeleo Chadema, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu kujibu mashtaka ya kufanyaka mkusanyiko/maandamano yasiyo halali yenye vurugu na uchochezi wa chuki kinyume na sheria.
Hivyo makala MBUNGE CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO
yaani makala yote MBUNGE CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mbunge-chadema-afikishwa-mahakama-ya.html
0 Response to "MBUNGE CHADEMA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO"
Post a Comment