title : Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar.
kiungo : Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na kumalizika kwa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang'ombe kwa Amani na Utulivu na kuwapongeza Wananchi wa Jang'ombe kwa utulivu wao.
Na Mwashungi Tahir Maelezo 31-10-2018.
MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud amewapongeza wananchi wa Jimbo la Jang’ombe kwa kufanya uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo kwa amani na utulivu mkubwa.
Ameyasema hayo Ofisini kwake Vuga wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu uchaguzi mdogo wa Jimbo la hilo uliofanyika tarehe 27.10.2018 ambapo mgombea wa CCM Ramadhan Hamza Chande alishinda kwa asilimia 90.5 ya kura zilizopigwa.
Alitoa shukurani za dhati kwa wananchi wa jimbo la Jangombe kwa kuonyesha ustaarabu mkubwa kuanzia kipindi cha kampeni hadi wakati wa kupiga kura na hatimae kupatikana mshindi.
Alisema kabla ya kuanza kwa kampeni wananchi niliwaomba kudumisha amani na wao wamenisikiliza na kutumia haki yao ya demokrasia kwa utulivu mkubwa, ningependa kuona ustaarabu kama huo unaendelezwa mpaka kwenye uchuguzi mkuu wa mwaka 2020.
“Tumezowea kuona vurugu wakati wa kipindi cha kampeni na uchaguzi , lakini uchaguzi huu mdogo wa Jimbo la Jang’ombe umekuwa wa amani nawaomba ustaarabu wa aina hii uendelee kwenye chaguzi nyengine zijazo, “ Alisema Mkuu wa Mkoa.
Aidha alieleza kuridhishwa na usimamizi mzuri wa Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC), vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na vyombo vya habari kwa mchango wao mkubwa uliopelekea kufanikisha uchaguzi wa Jimbo hilo ambapo wagombea wote wameridhika na kuyakubali matokeo .
Aliwaeleza wananchi wa Jimbo hilo kuwa uchaguzi umekwisha na mgombea amepatikana hivyo watu waendelee na majukumu yao ya kutafuta maisha na kumtakia kheri mwakilishi wa jimbo hilo Ramadhani Hamza Chande.
“Uchaguzi umekwisha nawaomba wananchi muendelee na kazi zenu za kujiletea maendeleo na sio kukaa vijiweni kuzungumzia siasa,”Alisisitiza Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud.
Amemtaka mwakilishi huyo mpya kutekeleza majukumu yake kwa kutumia ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuwa na mshirikiano na wananchi pamoja na viongozi wenziwe.
caption
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayuob Mohamed Mahamuod akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Vuga kuhusu hali ya amani na utulivu wakati wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jang’ombe uliofanyika tarehe 27/10/2018 (Picha na Kijakazi Abdalla Habari Maelezo)
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar
Hivyo makala Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar.
yaani makala yote Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mkuu-wa-mkoa-wa-mjini-magharibi-unguja_31.html
0 Response to "Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud Akizungumza na Waandishi wa Habari Zanzibar."
Post a Comment