MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU

MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU
kiungo : MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU

soma pia


MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU


Na Ramadhani Juma ,Ofisi ya Mkurugenzi

HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma kupitia Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu imeendelea kuimarisha miundombinu ya usafi kwa kuongeza vifaa vya kutunza uchafu katika mitaa kadhaa ya Mji ili kuhakikisha Wananchi hawatupi taka ovyo.

Akizungumza wakati wa uwekji wa vifaa hivyo, Mkuu wa Idara hiyo Dickson Kimaro alisema Manispaa inatarajia kuongeza ‘vitunza uchafu’ 11 katika mitaa mbalimbali ili kuweka mazingira rafiki ya kutunza uchafu kwa Wakazi wa Mji wanaokuwa katika shughuli zao za kila siku.

“Hizi ni juhudi za makusudi ili kuhakikisha Mji wetu unakuwa safi muda wote…natoa wito kwa Wakazi wa Manispaa yetu watumie vifaa hivi kuhifadhia uchafu mdogo wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku” alisema Kimaro.

Alisema mbali na vifaa hivyo, tayari Manispaa ilishasambaza vifaa vikubwa vya kukusanyia taka za aina zote (Skip Bucket) 61 katika Kata mbalimbali zinazotumika kama vituo vya kukusanyia taka kabla ya kubebwa na Mitambo ya Manispaa na kupelekwa katika Dampo la Kisasa lililopo eneo la Chidaya Kata ya Matumbulu nje kidogo ya Mji.



Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu wa Manispaa ya Dodoma Dickson Kimaro akikagua moja ya vifaa vipya vilivyowekwa katika Mtaa wa Kuu kwa ajili kutunza uchafu ikiwa ni juhudi za Manispaa hiyo kuhakikisha Mji unakuwa safi wakati wote.

Moja ya vifaa vya kutunzia taka (kulia) kilichopo mkabala na Viwanja vya Nyerere katikati ya Mji wa Dodoma


Hivyo makala MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU

yaani makala yote MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/manispaa-yazidi-kuingarisha-makao-makuu.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MANISPAA YAZIDI KUING’ARISHA MAKAO MAKUU"

Post a Comment