title : HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY
kiungo : HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY
HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imekosa mashine ya X-RAY ,hali inayosababisha matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila.
Akizungumza na Michuzi blog, Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo ameeleza ujenzi wa hospitali ya Mkamba unaendelea vizuri hadi sasa nyumba ya mganga, chumba cha upasuaji, maabara na wodi ya wazazi zipo katika hatua nzuri na hii ni kwa msaada wa serikali.
Mwandambo ameeleza wanapokea akina zaidi ya 300 kwa ajili ya kujifungua, hivyo ujenzi wa hospitali ya Mkamba utapunguza adha hiyo.Aidha meeleza kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa mashine ya X-RAY tangu ilipoanzishwa na bado wanapambana na wadau mbalimbali akiwemo Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega ili kutatua changamoto hiyo.
Pia amefafanua kuwa rufaa za kokosa damu zimepungua kutoka asilimia 28 hadi asilimia 3 na bado wanaendelea kuelimisha wananchi kuhusu kulima na kula mboga za majani sambamba na matumizi ya dawa za kuongeza damu kwa wajawazito.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde ameeleza madaktari wapo ila hawana mashine ya X-RAY hali inayowagharimu kuwapeleka wagonjwa hospitali nyingine.
Aidha Munde amesema madaktari wapo na chumba cha X-RAY kipo tayari kwa kutegemea mashine kutoka kwa Wizara husika lakini bado ni kitendawili.Pia Munde ameongeza mwaka jana Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Ulega walikuwa na maongezi na aliyekuwa Balozi wa China nchini kuhusu kupatikana kwa mashine hiyo.
"Na maongezi hayo yana matumaini kidogo baada ya kufika muafaka wa balozi huyo kuchangia fedha kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo,"amesema.Amefafanua kama Halmashauri wanatakiwa kuchangia dola za Marekani 40,000 ambazo zinatakiwa zilipwe kwa wasambazaji ndipo dola 30,000 zitolewa na balozi wa China kwa ajili ya ununuzi wa mashine hiyo.
Muonekano wa majengo ya kituo cha Afya Mkamba wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Steven Mwandambo akizungumza na Michuzi Blog kuhusu Hosptal ya Wilaya kukosa mashine ya X-RAY,hali inayosabaisha matumizi makubwa ya fedha kwa kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Taifa Mhimbili na Mloganzila.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga Eng. Mshamu Munde akizungumza na Michuzi Blog kuhusu kukosekana kwa huduma ya mashine ya X-RAY ,hali inayowagharimu kuwapeleka wagonjwa katika hospitali nyingine.(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.
Hivyo makala HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY
yaani makala yote HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/hospitali-wilayani-mkuranga-yakosa.html
0 Response to "HOSPITALI WILAYANI MKURANGA YAKOSA MASHINE YA X-RAY"
Post a Comment