title : WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA
kiungo : WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA
WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA
* Ni baada ya kumalizika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
RAIS Dkt. John Magufuli amewaasa Waislam na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kutenda mema baada ya kuwa wamejisahihisha na kutubu makosa yao ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Juni 15, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. Magufuli kwenye Baraza la Eid El Fitr lililofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema Viongozi wanaendelea kuwasihi Waislam wote na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuonesha upendo, umoja na kuvumiliana hasa baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Amesema huruma, ukarimu na ucha Mungu ulioneshwa katika kipindi cha mfungo wa ramadhani, uendelee na uwe sehemu ya maisha ya kila siku na kamwe usiwe umeisha baada ya mwandamo wa mwezi wa mfungo mosi.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa upendo, umoja, utulivu, mshikamano na subra uliooneshwa kipindi chote cha mfungo wa ramadhani ni vema ukaendelezwa kwa sababu ucha Mungu si katika mwezi huo pekee.
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameniagiza kwa kusema ‘’Waislam ni kielelezo cha taasisi za dini zinazozingatia maadili mema, hivyo wachache wasijipenyeze na kuharibu taswira yao. Ninawahakikishia kuwa Serikali iko tayari kushirikiana taasisi yeyote ya dini ambayo itakuwa tayari kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na taratibu tulizojiwekea nchini’’
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (wapili kulia) na Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salim (wapili kushoto) baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Baraza la Eid, Juni 15, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kushoto) kuingia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika Baraza la Eid Juni 15, 2018. Wapili kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salim.
Baadhi ya waliohudhuria katika Baraza la Eid wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Baraza hilo akimwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Juni 15, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA
yaani makala yote WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/06/watanzania-watakiwa-kuendeleza-matendo.html
0 Response to "WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEZA MATENDO MEMA"
Post a Comment