Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu

Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu
kiungo : Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu

soma pia


Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu

KITUO cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kitaendelea kutroa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na ofisi zote zinazofabnya shughuli zake kwenye kiwanja hicho. 

Mkuu wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Juma Yange amesema leo wakati wa kufunga mafunzo ya zimamoto na uokoaji yaliyofanyika kwa washiriki kupata nadharia na baadaye vitendo yaliyofanyika katika maeneo ya kiwanja hicho. 

Afande Yange amesema kwa kuwa wafanyakazi wengi hawajui namna ya kujiokoa wakati wa majanga ya moto, sasa watafanya mafunzo hayo kuwa endelevu kwa kufanya mara kwa mara, endapo moto utatokea basi waweze kujiokoa na kuokoa mali. 

“Mafunzo haya madhumuni yake makubwa ni ili kila mfanyakazi aelewe umuhimu wa kuwa makini dhidi ya adui moto kwenye sehemu yake ya kazi, kufahamu vyanzo na vitu vinavyosababisha moto a vifaa vya huduma ya kwanza vya kuzimia moto vilivyopo eneo lake la kazi, hivyo litakuwa endelevu,” amesema. 
 Kamishna Msaidizi wa Zimamoto, Hamis Telemkeni (mbele) akitoa maelezo kwa  washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuzima moto yaliyofanyika kwenye Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) leo.

 Mkaguzi Zimamoto Theresia Tengia  (kushoto) na Sajini Maria Gulam (kulia) wakionesha wafanyakazi wa ofisi mbalimbali zinazoendesha shughuli zake kwenye Kuiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), moja ya kifaa aina ya blanketi linalosaidia kuzima na kufunika  moto endapo utatokea bila kumuathiri kwa kuungua.

 Sajini Maria Gulam (mbele) akionesha namna ya kutumia mtungi wa kuzimia moto kwa washiriki wa mafunzo ya uzimaji moto na uokoaji yaliyofanyika leo kwenye Kituo cha Zimamoto kilichopo katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

 Bi. Julieth Fonga (kushoto) wa Kampuni ya General Aviation Services iliyopo Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akielekezwa na Afisa Usalama wa Zimamoto na Uokoaji, Leonard Chami namna ya kuzima moto kwa kutumia mtungi, wakati wa mafunzo yaliyofanyika leo kwenye kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha JNIA.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu

yaani makala yote Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/zimamoto-jnia-kutoa-mafunzo-endelevu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Zimamoto JNIA kutoa mafunzo endelevu"

Post a Comment