Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote

Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote
kiungo : Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote

soma pia


Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote

Mwambawahabari 


MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewasilisha taarifa ya Utekelezaji  wa Ilani ya ccm ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 hadi 2017 akiwasilisha taarifa hiyo Sophia Mjema alisema katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020 Chama cha mapinduzi itachukua dola.
Mjema alisema katika wilaya ya Ilala   chama cha mapinduzi   itashinda  chaguzi za Kata na kuzoa viti vya ubunge vyote    na kuendelea kushika dola .


"Wilaya ya Ilala kwa sasa INA madiwani 49 katika baraza la madiwani kati ya madiwani 49, Madiwani 17 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA , madiwani 21 wa Chama cha Mapinduzi CCM na madiwani saba wa Chama cha Wananchi CUF   na Wabunge watatu " alisema Mjema.



Mjema amesema hali ya kisiasa kwa sasa Wilaya ya Ilala safi    katika utekelezaji wa Ilani .

Akielezea muundo wa Utawala wilaya hiyo INA tarafa TATU kata 36 na mitaa  159, tarafa ya KARIAKOO ina kata kata 13 mitaa 23, Tarafa ya Ilala kata 14 mitaa 75 na tarafa ya Ukonga Kata 9 mitaa 61 majimbo ya uchaguzi matatu
Ilala kata 10, Ukonga Kata 13 na Jimbo la SEGEREA kata 13.

Amesema katika Wilaya hiyo kwa mujibu wa sensa ya makazi iliyofanyika Kitaifa 2012 wilaya INA wakazi jumla 1,220 , 611 wakiwemo Wanaume 595,928 na WANAWAKE 624,683 kufuatia ongezeko la Watu la asilimia 5.6 kwa mwaka kwa sasa 2016 idadi ya wakazi inakadiriwa kufikia 1, 515,359
Wanaume 739,830 na WANAWAKE 775,529.

Akizungumzia shughuli za kiuchumi kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) inakadiriwa kuwa asilimia 43,97 ya wakazi wa Ilala wameajiliwa katika sekta binafsi na sekta ya Umma  na asilimia 56 .03 wamejiajili wenyewe na katika sekta binafsi wanajishughulisha na shughuli ndogondogo uvuvi ,kilimo na ufugaji wastani wa pato la mkazi wa wilaya hiyo ni sh. 1,73 4,842 kwa mwaka.

" Utekelezaji wa mpango wa Ilani sekta ya fedha kwa mwaka wa fedha 2017 hadi 2018 mpango wa Ilani umelenga kuendelea kuboresha takwimu za Walipa kodi wetu kutoka katika chanzo cha Mapato  kuendelea kununua vitendea kazi hususani magari ya kufuatilia mapato na vifaa vya Kielektroniki vya kupokelea mapato, Kukusanya jumla ya  sh, 59 , 991 kutoka vyanzo vya ndani" alisema .

 Mjema akielezea sekta ya huduma za jamii katika kutekeleza Ilani ya mwaka 2017 hadi 2018 mpango umelenga kuandikisha watoto 7,460,wa Shule za awali na watoto 19, 705 darasa la kwanza  katika shule   za msingi  na kununua madawati 2000, ujenzi wa vyumba vya madarasa 50,matundu ya vyoo 145 na ujenzi wa OFISI nane  za Walimu .

   Wakati huohuo Sophia Mjema amemtaka Mkurugenzi wa Ilala kuwachukulia hatua Wenyeviti wa Mtaa wanaotoza  sh.2000, hadi 5000 kwa wananchi wakienda kuomba Barua ya utamburisho bila kujali chama anachotoka iwe CCM au chama cha upinzani kwani utawala bora hauruhusu kuwahudumia wananchi kwa malipo.

Amewagiza Wajumbe wa Halmashauri kuu kuchukua rekodi ya Wenyeviti wa Mtaa wenye tabia  hiyo.


Hivyo makala Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote

yaani makala yote Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wilaya-ya-ilala-2020-itachukua-majimbo.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wilaya ya Ilala 2020 itachukua majimbo yote"

Post a Comment