title : WASICHANA WALIOTEKWA WAREJESHWA NYUMBANI
kiungo : WASICHANA WALIOTEKWA WAREJESHWA NYUMBANI
WASICHANA WALIOTEKWA WAREJESHWA NYUMBANI
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
WANAFUNZI wa kike 110 waliotekwa February 19 katika shule ya bweni Dapchi nchini Nigeria wamerejeshwa nyumbani kutoka kwenye mikono ya waasi.
Waziri wa habari nchini humo Alhaj Lai Mohammed ameeleza kuwa wanafunzi 101 kati ya 110 wamerejeshwa salama na hiyo ni baada ya jeshi kuweka juhudi ili kunusuru maisha ya watoto hao.
Licha ya Wizara kutothibitisha inasemekana wasichana watano wamefariki dunia na hiyo ni kutokana na maeleza ya Aisha Kachalla Bukar (14) mmoja wa manusura hao aliyoyatoa kwa baba yake.
Pia inasadikika kuwa mmoja wa wanafunzi hao(mkristo) bado anaendelea kushikiliwa na waasi hao baada ya kukataa kuslimu.Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari ameeleza kuwa janga la utekaji ni la kitaifa na ametoa pole kwa waathirika wote.
Ifahamike kuwa mwaka 2014 wanafunzi 300 walitekwa huko Chibok na hadi sasa wanafunzi 100 bado hawajapatikana.
Hivyo makala WASICHANA WALIOTEKWA WAREJESHWA NYUMBANI
yaani makala yote WASICHANA WALIOTEKWA WAREJESHWA NYUMBANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WASICHANA WALIOTEKWA WAREJESHWA NYUMBANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wasichana-waliotekwa-warejeshwa-nyumbani.html
0 Response to "WASICHANA WALIOTEKWA WAREJESHWA NYUMBANI"
Post a Comment