title : VIGOGO WATAO WA TPDC WAPANDISHWA KIZIMBANI
kiungo : VIGOGO WATAO WA TPDC WAPANDISHWA KIZIMBANI
VIGOGO WATAO WA TPDC WAPANDISHWA KIZIMBANI
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
Wakurugenzi watano waliokuwa wa shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC), akiwemo, Mkurugenzi mtendaji James Mataragio na wenzake wanne, leo Machi, 16, 2018 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ya zaidi ya bilioni 7.
Mbali na Mataragio, washtakiwa wengine ni Mkurugenzi wa fedha, George Seni, Welington Hudson, Mkurugenzi wa mkondo wa juu, Kelvin Komba, na Mkurugenzi wa manunuzi na Ugavi, Edwin Riwa.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali kutoka Takukuru, Emmanuel Jacob amedai, kati ya April 8, 2015 na June 3, 2016 washtakiwa hao wakiwa Watumishi wa umma na waajiriwa wa Shirika la Maendeleo la Petrol (TPDC), katika nafasi zao hizo za kazi walitenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.

Hata hivyo, washtakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama waliyopewa na Mahakama.
Mahakama imewataka kuwa na wadhamini wawili watakai saini bondi ya bilioni moja kila mmoja huku washtakiwa wenyewe nao wakitakiwa kusaini bondi hiyo ya bilioni moja. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 19, mwaka huu.
Hivyo makala VIGOGO WATAO WA TPDC WAPANDISHWA KIZIMBANI
yaani makala yote VIGOGO WATAO WA TPDC WAPANDISHWA KIZIMBANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIGOGO WATAO WA TPDC WAPANDISHWA KIZIMBANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/vigogo-watao-wa-tpdc-wapandishwa.html
0 Response to "VIGOGO WATAO WA TPDC WAPANDISHWA KIZIMBANI"
Post a Comment