title : BENKI YA TIB COORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA
kiungo : BENKI YA TIB COORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA
BENKI YA TIB COORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Benki ya TIB Coorporate imewataka wananchii kujitokeza kwenye banda lao lililopo ndani ya maonesho ya 42 ya Sabasaba na kuweza kufungua akaunti za benki hiyo ili waweze kujivunia faida kibao kwa kuweka hela zao Kwenye benki ya TIB.
Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Coorporate Theresia Msoka amesema kuwa Benki ya TIB Coorporate imezindua aina tofauti nne za akaunti ambazo zitamuwezesha mteja wa benki hiyo kufungua akaunti na kuhifadhi fedha zake kwa uhakika zaidi.
Amesema kuwa benki yao ni ya kibiashara ila inawahudumia wananchi wote wakiwemo watu binafsi, taasisi au makampuni pamoja na kuwawezesha kupata mikopo ya haraka sana kwa ajili ya kufungua au kuendeleza biashara zao ikiwemo viwanda.
Bi Theresia amesema kwa mwaka huu wamekuja na kauli mbili ya "JIPANGE NA TIB COORPORATE BANK" ambao wamewaletea akaunti nne tofauti zitakazomuwezesha mwananchi kuhifadhi fedha zake na kujipatia riba kubwa zaidi kadri anavyoweka hela ukiweka fedha kwenye akaunti ya Flex inayopatikana ndani ya benki yao.
Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Coorporate Theresia Soka akielezea
Meneja wa Fedha wa Benki ya TIB Coorporate June Magingi na Ofisa huduma kwa wateja Janeth Burton (kulia) Wakimpatia maelekezo mteja aliyefika katika banda lao la maonyesho lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya Masasi Food Production Secky Nyewa akielezea namna Benki ya TIB ilivyoweza kuwapatia mkopo na kuwezesha kufungua kwa kiwanda hicho kinachotengeneza bidhaa za chakula ndani ya maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akielezea jambo mbele ya Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko Theresia Soka wa Benki ya TIB Coorporate (kushoto) na Mkuu wa Utafiti wa Maendeleo ya Benki TIB Coorporate Dr Hildebrand Shayo alipotembelea banda ya benki hiyo ndani ya maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya TIB Coorporate wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda lao la Maonyesho kwenye Viwanja vya Sabasaba maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Matawi na Masoko Benki ya TIB Coorporate Theresia Soka akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi alipotembelea banda la maonyesho la benki ya TIB lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Utafiti wa Maendeleo ya Benki TIB Coorporate Dr Hildebrand Shayo akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi alipotembelea banda la maonyesho la benki ya TIB lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BENKI YA TIB COORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA
yaani makala yote BENKI YA TIB COORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA TIB COORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/benki-ya-tib-coorporate-yawataka.html
0 Response to "BENKI YA TIB COORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA"
Post a Comment